Sababu kuu kwa nini wanafunzi katika Kampasi wangependelea masomo ya mitandaoni

Muhtasari
  • Hapo awali, hakukuwa na kitu kama masomo ya mtandaoni kwa kuwa teknolojia haikuwa ya hali ya ju

Mlipuko wa COVID 19 ulikuja na athari kadhaa na moja kubwa zaidi ni kwamba kila kitu kilianza kufanya kazi mtandaoni ulimwenguni.

 

Kazi ilifanyika nyumbani mtandaoni na pia walimu walibuni mifumo ya mtandaoni ambapo wanafunzi wangeweza kusoma wakiwa nyumbani au popote walipo. Teknolojia hii ilikuja na faida zake kama ilivyoelezwa hapa chini.

1. Masomo ya mtandaoni yaliokoa nauli ya mwanafunzi kwenda shuleni.

Kwa kuwa inakuwa si lazima kwa mwanafunzi kutembea kwa miguu kwenda shuleni au hata kupanda matatu kwenda shuleni, majukwaa ya mtandaoni yalimwezesha mwanafunzi kusoma kutoka mahali popote wakati wowote. Hii inaokoa pesa ambazo unaweza kutumia kwenda shuleni na kurudi na kuzitumia kwa kitu kingine.

2..Kuthamini teknolojia

Hapo awali, hakukuwa na kitu kama masomo ya mtandaoni kwa kuwa teknolojia haikuwa ya hali ya juu. Kufanya mambo mtandaoni kama vile masomo huthamini ukweli kwamba teknolojia imeendelea na hii huwasaidia wanafunzi kupata kujua mengi kuhusu teknolojia ya habari.

3,Huokoa wanafunzi kutokana na masuala ya usalama.

Wanafunzi wengi wanapoenda shuleni au wanaporudi huvamiwa njiani na kuibiwa pesa zao, simu au kompyuta zao za pajani. Ukiwa na madarasa ya mtandaoni, unatakiwa tu kuingia katika akaunti yako ya shule ya kujifunzia kielektroniki na kusoma popote pale. Hii inaweza kukuokoa. kutokana na drama nyingi za kuibiwa.

4.Hupendelea wanafunzi wenye matatizo ya kiafya

Kwa wanafunzi wengi, elimu ya mtandaoni ndiyo njia ya kuchagua. Inawafaa wanafunzi wenye ulemavu au matatizo ya kiafya kama vile wasiwasi wa kijamii au kukosa usingizi. Madarasa ya kitamaduni na mbinu za kujifunzia zinaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya wanafunzi, ilhali wanapendelea kujifunza mtandaoni au kuhudhuria madarasa kutoka kwa starehe ya nyumba zao.