Siku Ya Msaada wa Kibinadamu Duniani

Mwaka wa 2022, zaidi ya wafanyikazi 72 wamepoteza maisha yao.

Muhtasari

• Takwimu zinaonyesha kwamba , katika kipindi cha mwaka 2022 zaidi ya watu milioni 235 wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na athari mbalimbali za madaliko ya tabianchi.

Image: THE STAR

Siku ya msaada wa kibinadamu inayofanyika kila tarehe 19 mwezi wa nane, husherehekwa na wafadhili au watu ambao pakubwa wamejitosa katika kusaidia wasiojiweza.

Siku hii ilitengwa na umoja wa kimataifa[UN] mwaka wa 2009 kukumbuka shambulio la makazi yao katika taifa la Iraq.Watu kumi na wawili waliaga dunia ikiwemo mkurugenzi wa huduma za kibinadamu, Bw Sergio Viera de Mello.

Misaada hii husaidia wale wasiojiweza au wahasiriwa wa majanga kama vile Ukame, mashambulio ya kigaidi na tatizo la tabianchi.

Takwimu zinaonyesha kwamba , katika kipindi cha mwaka 2022 zaidi ya watu milioni 235 wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na athari mbalimbali za madaliko ya tabianchi.

Athari za mabadiliko ya tabianchi zinatishia usalama, ustawi na maendeleo ya wengi. Waathirika wa majanga asilia ni maskini.

Imeelezwa kuwa binadamu katika uhai wake ana vitu vingine anavyoweza kutumia au la lakini si hewa ambayo anahitaji wakati wote wa uhai uhai wake.Unahitaji msaada kutoka kwa wengine ndiposa kujikomoa toka kwa lindi la balaa.

Wahudumu wa mswala ya kibinadamu wako mstari wa mbele katika mchakato wa kuwasaidia kuokoa maisha ya watu ambao wako hatarini sehemu mbalimbali za dunia,majanga yanapozuka.Hawa ni watu wanaohatarisha maisha yao kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, matukio ya wafanyikazi hawa kupigwa risasi, kutekwa nyara na hata kunyanuaswa utu, heshima na haki zao yanazidi kushamiri. Mwaka wa 2022, zaidi ya wafanyikazi 72 wamepoteza maisha yao.

Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya kanisa Katoliki kimataifa, Caritas International limekuwa likihamasisha jumuiya ya kimataifa kujipanga kikamilifu ili kukabiliana na athari za majanga kama vile michafuko wa mashambulizi ya kigaidi nchini Afaghanstan na Lebanon.Pia inawataka wakuu wa jumuiya kutunga sera duniani, kuhakikisha kwamba usalama wa chakula ilikuepusha raia dhidi ya hatari ya njaa.

Ni wakati muafaka wa kurekebisha mifumo wa uchuni na malengo yake.Binadamu anapaswa kuchukua hatua ya kwanza kufanya wongofu wa kiikolojia na kwamba , kisaidie kujenga huruma kwa kujikita katika kipaji cha ubunifu na ujasiri.

Sera hii pia ilenge kuimarisha zaidi huduma na haki za wahudumu hawa maana jamii inawahitaji pakubwa sana.