Jamaa amuoa dadake na kupata watoto wanne pamoja

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa mwongo mmoja.

Muhtasari

•Paulen Ziarirwa mwenye umri wa miaka 28 alimuoa dadake mdogo Dorica Ziarirwa ,26, bila kujali uhusiano wao wa kifamilia.

•Paulen na Dorica walichagua kuhamia eneo la Kashegema ambako walianzisha familia yao.

Paulen Ziarirwa na Dorica Ziarirwa wakiwa na watoto wao wanne.
Arimax Paulen Ziarirwa na Dorica Ziarirwa wakiwa na watoto wao wanne.
Image: Youtube

Mwanamume mmoja kutoka Congo DRC amewashangaza wengi  baada ya kumuoa dada yake na kujaliwa watoto wanne pamoja.

Paulen Ziarirwa mwenye umri wa miaka 28 alimuoa dadake mdogo Dorica Ziarirwa ,26, bila kujali uhusiano wao wa kifamilia.

Wanandoa hao wanasema walizaliwa kijijini cha Bunio ambako kulikuwa na migogoro wa kikabila jambo lililowafanya wakaazi kuhamia kijiji cha Miti ambako kulionekana salama. Miongoni mwa waliohama kijijini Miti ni Paulen na dadake Dorica.

Huko katika kitogoji cha Miti walipokelewa na wasamaria wema ingawaje hawakukaa kwa muda mrefu.  Ndugu hao waliamua kurudi walikotoka Bunia kwa ajili ya kwenda kuwatafuta wazazi wao bila mafanikio.

Wawili hao walikaa kijijini kwao kwa muda mrefu na kutokana na upweke na msisimko wa mwili, Paulen alijawa na wawazo ya kutaka kumuoa dadake. Alimuuliza Dorica ikiwa angekubali ombi la kuwa bibi yake. Dorica bila kusita, alisema ingebidi wahamie eneo lingine kwani jamii yao ingewasema tokana na maamuzi yao.

Paulen na Dorica walichagua kuhamia eneo la Kashegema ambako walianzisha familia yao. Wanandoa hao sasa wanajivunia kuitwa baba na mama wa watoto 4.

Pauline anasema  ''ninapomwona mtoto wangu wa kwanza mwenye miaka 8 sasa huwa nafurahia kwa sababu nampenda''

Paulen ambaye amekuwa kwenye ndoa na dadake kwa miaka 10, anasema katu hajutii kumuoa. Anasema siri kubwa ambayo amehifadhi ni kutowaambia watoto wake kuhusu historia yao ya hapo mbeleni ila atawajulisha watakapokuwa watu wazima.

''Tunajaribu kwa kila namna tuwezavyo ili watoto wetu wasijue chochote kuhusu sisi. Hatutaki wajue kuwa sisi ni ndugu na dada.'' Pauline alieleza.

Dorica anasema wanaishi kwa amani na upendo kwani wanafahamiana vizuri hivyo hakuna anayeshuku mwingine kwa madai ya kuchezeana au kusalitiana.

Dorica aliendelea na kusema kuwa hata kama familia yake itapata kujua ndoa yao bado hawataachana kwani wanapendana sana.