Nilipata ameoa baada ya kutoka jela-Mwanamke asimulia

Kwa hakika kila mmoja ana hadithi ya kusimulia kuhusu maisha yao, kwa kile wamepitia na kuona.

Muhtasari
  • Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na mwanamke, ambaye ana hadithi ya ajabu kuhusu maisha yake
  • Monicah ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa, kwa kosa ambalo hakutarajia kwamba angepatana na mkono wa sheria, alisimulia jinsi mumewe alimsaliti
Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Katika maisha ya kila mwanadamu kuna baadhi ya changamoto ambazo wanapitia licha ya kuamka kila siku na kusukuma gurudumu la maisha.

Kwa hakika kila mmoja ana hadithi ya kusimulia kuhusu maisha yao, kwa kile wamepitia na kuona.

Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na mwanamke, ambaye ana hadithi ya ajabu kuhusu maisha yake.

Monicah ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa, kwa kosa ambalo hakutarajia kwamba angepatana na mkono wa sheria, alisimulia jinsi mumewe alimsaliti.

"Mume wangu alikuwa ameniacha nyumbani pekeyangu wakati huo sikuwa nimemaliza miaka 5 katika ndoa wacha niseme nilikuwa mwanamke wa umri wa 29, ndugu yake alinitembelea na kujaribu kunibaka jambo ambalo nilichukua kisu na kumdunga ilhali hakufa

Baada ya tukio ndugu yake alisema kwamba nilikuwa nataka kumuua, na wala hakufanya jambo lolote na kwamba nimepagawa, bila ya kujua hivyo ndivyo nilifungwa jela kwa makosa ya kujaribu kuua

Kwa mwaka mmoja na nusu mume wangu alinitembelea na kunitia moyo, baada ya hapo sikuweza kumuona tena wala kusikia jina lake, baada ya kumaliza kifungo changu nilipata amemuoa mwanamke mwingine, na walahakujali nilichokuwa napitia nikiwa jela

Hakuonyesha kitendo cha kuniomba msamaha, badala yake alinikemea na kuniambia nirudi jela kwa kuwa mimi ni muuaji,"Alieleza Monicah.

Cha kusikitisha zaidi ni kuwa Monicah alipata wanawe wamefukuzwa na mwanamke huyo.

"Jambo ambalo liliniuma ni kuwa mwanamke huyo aliwafukuza watoto wangu wawili  wakiwa na umri wa chini na hakujali wataenda wapi, walielekea kwa ddada yangu ambaye aliwalea kama watoto wake, ningekuwa nataka kulipiza kisasi lakini Mungu alinionekania licha yamakovu yangu, sasa nashukuru Mungu kwa yale nilipitia kwani yamekuwa hadithi ya maisha yangu."