Mfahamu jamaa aliyegoma kuzungumza kwa miaka 17, asema ilimpa amani ya moyo

John Francis alikataa kuzungumza baada ya kuona mafuta yakimwagika mjini wa San Francisco na kuharibu mazingira

Muhtasari

• Aliamua kufunza mazungumzo ya ishara kama njia ya mawasiliano ili watu wasije wakamwona kama kichaa.

John Francis aliamua kutozugumza tangu mwaka wa 1973
John Francis aliamua kutozugumza tangu mwaka wa 1973
Image: BBC

Katika ulimwengu wa sasa ni binadamu yupi ambaye anayeweza kukata kauli ya kutozungumza na mwenzake sio kwa saa moja au kwa siku bali kwa miaka17?

Lakini kwake John Francis, mzaliwa wa Marekani alikata kauli ya kutozungumza na mtu yeyote tangu mwaka wa 1973 alipokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Alikataa kuzugumza kwa sababu ya ajali ya kumwagika kwa mafuta mji wa  San Francisco mwaka wa 1971 iliyofanya uharibifu mkubwa wa mazigira, wanyama na hata kuathiri binadamu.

Ajali hiyo ilimfanya kusomea kozi ya mazingira na kuamua kutowahi kutumia magari kama njia ya kutochangia katika uharibifu wa mazingira kwa vyovyote vile.  Aliamua kutembea nchi mbali mbali za ulimwengu huku akifoka na kuhubiri manufaa ya kuwa na mazingira safi hadi watu wakambatiza jina Planetwalker.

Kwa wiki ya kwanza watu walimwona kama alikuwa anajipendekeza au hataweza kustahimili kutozungumza na mtu ila kwake Francis alikuwa amekata kauti ya kudumu. 

Familia yake ilijaribu juu chini kumshawishi kubadilisha nia yake ila hawakufanikiwa.

Hata mkewe ambaye alijawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa na tabia ya mumewe alikuwa alimetishia kumwacha bwanake iwapo ataendela kuwa kimya.

Aliamua kufunza mazungumzo ya ishara kama njia ya mawasiliano ili watu wasije wakamwona kama kichaa.

Baada ya miaka 17 ya kutozungumza, wakati watu walikuwa wamekongamana mkahawani jiji la Washington DC, alijawa na msisimko wa ndani wa kutaka kusema jambo.

Aliamua kunasa umakinifu wa watu na kutamka maneno yake ya kwanza. Alisema huku akicheka kuwa ''Asante kwa kufika hapa''  Matamshi haya yalishabikiwa na babake ambaye alikuwa amefurahishwaa kwa kusikia sauti ya mwanawe tena na sauti iliyokuwa tofauti na hapo mwanzo.

Baada ya kusikilizwa na maelfu ya watu,aliamua kuchukua muda huo mwafaka wa kutaka watu wajue mazingira ni nini.