Papa John Paul II alikuwa anajua mapadre walawiti, lakini aliwaficha ripoti

Ripoti hiyo inafichua kwamba John Paul kipindi akiwa Kadinali aliambiwa kuhusu mapadre waliokuwa wakiwallawiti watoto wavulana lakini aliwaficha.

Muhtasari

• Ripoti hiyo inaonesha wakati akiwa kadinali katika kanisa katoliki nchini Poland, alipokea malalamishi mengi ya ulawiti lakini hakuwachukulia hatua mapadre husika.

Papa John Paul wa pili
Papa John Paul wa pili
Image: BBC NEWS

Aliyekuwa papa wa kanisa katoliki hayati John Paul alificha unyanyaswaji wa watoto kipindi akiwa kama papa, ripoti mpya imeonesha kulingana na majarida ya kitaifa.

Kulingana na ripoti moja iliyopeperushwa kwenye runinga ya TVN Jumapili jioni, Papa John Paul wa pili alikuwa anajua kuhusu unyanyasaji wa watoto katika kanisa la katoliki nyumbani kwao Poland lakini kipindi chote alificha hayo matukio.

Michal Gutowski, mpelelezi nyuma ya ufichuzi huo, alisema kwamba Karol Wojtyla, kama alivyokuwa akiitwa kabla ya kuwa Papa wakati huo, alijua kuhusu kesi za makasisi wanaolawiti watoto ndani ya kanisa alipokuwa bado kadinali huko Krakow. Aliwahamisha mapadre kwa dayosisi nyingine -- moja mbali kama Austria -- ili kuhakikisha hakuna kashfa yoyote iliyotokea, alisema, AFP walisema.

Wojtyla, ambaye alikuwa papa kwa miaka 27 kuanzia 1978 hadi kifo chake mwaka 2005, aliandika barua ya mapendekezo kwa kasisi anayetuhumiwa kwa unyanyasaji kwa kadinali wa Vienna Franz Koenig, bila kutaja shutuma hizo, anasema Gutowski kweney ripoti hiyo.

Wakati wa uchunguzi wake, mpelelezi huyo kwenye runinga alisema alizungumza na waathiriwa wa makasisi wanaolawiti watoto, familia zao na wafanyikazi wa zamani wa dayosisi ya kanisa.

Mpelelezio huyo kulingana na ripoti hiyo alisema kwamba kanisa lilimnyima idhini ya kufanyia uchunguzi nyaraka za marehemu John Paul.

Kanisa la Poland hapo awali lilikataa kutoa hati kwa mahakama au tume ya umma ya uchunguzi inayochunguza kesi za unyanyasaji wa watoto kanisani.

Waathirika kadhaa waliozungumza kwenye Makala hiyo na ambao hawakutana majina au sura zao kuweka wazi walikiri kutoa taarifa za makasisi waliokuwa wakiwalawiti watoto wavulana kwa papa John Paul lakini hakuwahi zingatia wala kuchukua hatua zozote za kinidhamu na kisheria.