Wanaume watembea kilomita 120 kutafuta wake

Lakini baadhi ya wanawake wanapendelea kuhamia maeneo ya mjini kwa sababu hiyo inatoa fursa zaidi za uhuru.

Muhtasari
  • Huku wanaume hao walipokuwa wakielekea katika hekalu, kundi lengine la wakulima katika eneo hilo lilikuwa likiandamana likidai bei nzuri ya bidhaa za miwa
Image: BBC

Mwezi uliopita, kundi la wanaume katika jimbo la kusini mwa India la Karnataka walitembea kilomita 120 kufikia hekalu ili waweze kuomba mungu wapate wake wa kuoa.

Juhudi hizo zimezua ucheshi mwingi mitandaoni, lakini wanaharakati wanasema inaangazia masuala ya ndani ya kijamii na kiuchumi eneo hilo.

Wanaume wengi waliojiunga na msafara huo ulioanza na wanaume 30 na kumalizika na 60, ni wakulima kutoka wilaya ya Mandya ya Karnataka.

Kwa miongo kadhaa, eneo hilo limekabiliwa na kiwango cha juu cha kuzaliwa kwa wanaume kuliko wanawake, na wanakampeni wanasema hii ni moja ya sababu kwa nini wanaume wengi wanapata shida kuoa.

Mambo mengine ni pamoja na kupungua kwa mapato ya kilimo Pamoja na wanawake kuwa na njia nyengine za kujikimu kuliko vizazi vilivyopita.

Malisha DB alikuwa mmoja wa walioshiriki msafara huo hadi katika Hekalu la Malli ya Mahadeshwara, ambalo wafuasi wake wanaamini maombi yao yatajibiwa.

"Wakati nilipaswa kutafuta mapenzi, nilikuwa na shughulika sana na kazi yangu. nilipata pesa na sasa kwa kuwa nina kila kitu maishani siwezi kupata msichana wa kuoa,” Malisha alisema.

Malisha ana miaka 33 pekee, lakini anasema tayari amepita umri unaofaa wa kuoa katika eneo lake.

Shivaprasad, mmoja wa waandalizi wa msafara huo, alisema kuwa zaidi ya wanaume 200 walijiandikisha kujiunga walipotangaza kwa mara ya kwanza. "lakini wengi walijitoa kwa sababu vyombo vya habari nchini humo viliripoti tukio hilo kwa njia hasi", Shivaprasad aliongezea.

Mandya ni eneo lenye rutuba na maji mengi ya kunyunyizia mimea shambani na miwa ni moja ya zao kuu linalolimwa eneo hilo. Lakini kipato kidogo cha wakulima kiliifanya taaluma hiyo kutodhaminiwa na wengi.

"Watu wanafikiri kwamba vijana kutoka katika familia za wakulima hawana kipato cha kujikimu," alisema Krishna, mwenye miaka 31, ambaye mi mmoja wa washiriki.

Malisha alisema katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita amekataliwa na wanawake takriban 30 ambao walisema taaluma yake na kuishi kijijini ni sababu za kutomkubali.

Huku wanaume hao walipokuwa wakielekea katika hekalu, kundi lengine la wakulima katika eneo hilo lilikuwa likiandamana likidai bei nzuri ya bidhaa za miwa.

Hata hivyo wanaharakati pia wanalaumu maoni ya mfumo dume kwa kutokuwa na usawa katika maswala ya uzazi.

"Hata baada ya upimaji wa kutambua jinsia ya mtoto anaezaliwa kupigwa marufuku mwaka wa 1994, utoaji mimba wa kutegemea jinsia uliendelea katika maeneo hayo," alisema Nagrivaka, mwanaharakati nchini humo.

katika shule, utapata mgao wa wanafunzi ni wasichana 20 kwa wavulana 80," aliongeza.

Kulingana na takwimu za hivi punde za zoezi la kuhesabu watu la sensa, mgao wa wanaume kwa wanawake huko Mandya ulikuwa wanawake 960 kwa wanaume 1,000 mwaka 2011, ikilinganishwa na wanawake 971 kwa kila wanaume 1,000 mwaka 2001.

Wanawake pia hufanya maamuzi tofauti. Jayashila Prakash, ambaye anatokea eneo la Mandya lakini sasa anaishi na familia yake maeneo ya nje ya vijijini ya Bengaluru, anasema " yeye binafsi" anapendelea kuishi katika kijiji kwa sababu ina mambo maengi ya asilia na ni rahisi kufanya urafiki na kuwa na uhusiano mzuri na watu.

Lakini baadhi ya wanawake wanapendelea kuhamia maeneo ya mjini kwa sababu hiyo inatoa fursa zaidi za uhuru.

"Ikiwa wanawake wataolewa na wakulima, itabidi wapate ruhusa kutoka kwa waume zao kutoka kwenda kufanya shughuli zao," aliongeza. "Katika kizazi chetu hakuna mtu anataka kumtegemea mwengine kwa hali hiyo."