logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mume wangu anataka watoto 10" Vera Sidika azungumzia mipango ya kupanua familia

Mama huyo wa binti mmoja alidokeza kwamba atafikiria kupanua familia yake tena baada ya miaka sita.

image
na Radio Jambo

Habari14 February 2023 - 03:55

Muhtasari


•Mama huyo wa binti mmoja alidokeza kwamba atafikiria kupanua familia yake tena baada ya miaka sita.

•Pia alifichua kuwa mtoto wake wa pili anayetarajia hivi karibuni atakuwa na chumba chake pekee yake.

Mwanasholaiti mashuhuri Vera Sidika ameweka wazi kwamba hana mpango wa kuongeza mtoto wa tatu hivi karibuni.

Wakati akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kwamba atafikiria kupanua familia yake tena baada ya miaka sita.

Vera Sidika hata hivyo alifichua kuwa mume wake, mwimbaji Brown Mauzo anataka sana wapate watoto kumi pamoja.

"Mume wangu anataka watoto kumi. Kwa upande wangu, sio wakati wowote hivi karibuni. Labda nitaongezea mwingine mmoja baadaye kabisa baada ya miaka sita," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo alikuwa akimjibu mtumizi mmoja wa Instagram ambaye alikuwa akitaka kujua ikiwaoanatazamia kuongeza watoto wengine baada ya kujifungua mtoto wake wa pili baadaye mwaka huu.

Wakati huohuo, Vera  alibainisha kuwa siku za hivi majuzi amekuwa bize katika majukumu yake ya kuwa mama wa mtoto, mfanyibiashara, kushughulikia ujauzito na pia kuhusika katika filamu ya Real Housewives of Nairobi.

Pia alifichua kuwa mtoto wake wa pili anayetarajia hivi karibuni atakuwa na chumba chake pekee yake.

"Asia na mtoto ambaye hajazaliwa watakuwa na vyumba tofauti bila shaka. Lakini kama kawaida, bado akiwa mtoto mchanga nitalala na yeye hadi afikishe miezi sita kisha ahame," alisema mke huyo wa Mauzo.

Wiki iliyopita, mjasiriamali huyo alifichua kwamba tayari amepanga siku ya kujifungua mtoto wake wa pili.

Vera aliweka wazi kuwa atajifungua mtoto wa pili kwa njia ya upasuaji kama ilivyokuwa na mtoto wake wa kwanza.

"Nimepanga tarehe ya upasuaji wa CS. Kama nilivyosema hapo awali napendelea CS. Hakuna Maumivu," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo alikuwa akiwashirikisha wafuasi wake katika kipindi  cha maswali na majibu kwenye Instagram.

Alipoulizwa kuhusu jinsia ya mtoto ambaye amebeba tumboni, mwanasoshalaiti huyo alidokeza kwamba pia yeye na mumewe hawajapata kutambua huku akiahidi kuandaa hafla kubwa  ya kufichua jinsia hivi karibuni.

"Itakuwa sherehe kubwa ya kufichua jinsia wakati huu. Siwezi kusubiri," alisema.

Vera pia alifichua kwamba yeye na mume wake Brown Mauzo hawakupanga ujauzito wa mtoto wao wa pili pamoja.

"Ilifanyika tu. Tuligundua ukiwa na miezi minne,

Aliweka wazi kuwa safari ya ujauzito wake wa pili imekuwa laini na hajakuwa akishuhudia dalili za ugonjwa wa asubuhi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved