Muhtasari
•Wakenya kote nchini waliadhimisha kuvuka mwaka kwa njia tofauti za kipekee
Kwaheri 2021, Karibu 2022.
Hatimaye tumeupungia mkono mwaka wa 2021 na kufungua kalenda mpya ya 2022.
2021 ulikuwa mwaka wa namna yake na ulikuwa na panda shuka zake. Kila mmoja wetu alisherehekea jambo fulani na kwa wakati mwingine tukapambana na hali fulani.
Wakenya kote nchini waliadhimisha kuvuka mwaka kwa njia tofauti za kipekee, wanawake kwa wanaume, wazee kwa wadogo.
Kunao baadhi ya Wakenya ambao walipendelea kuvukisha mwaka wakiwa kitandani, wengine vilabuni, wengine kanisani, wengine walikuwa safarini. Kila mmoja aliadhimisha hatua hiyo maalum kwa njia zake.
Haya hapa baadhi ya matukio katika mkesha wa mwaka mpya:-
Je, wewe ulisherehekea vipi ukiwa wapi?