Tazama picha za matayarisho ya mazishi ya mwanasiasa Mzee Kibor

Muhtasari
  • Marehemu atazikwa Aprili 1 nyumbani kwake karibu na Kabenes huko Uasin Gishu
  • Kibor alifariki wiki jana akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuishi maisha ya umma yenye utata
Image: Mathews Ndanyi

Maandalizi yako katika kasi ya juu kwa ajili ya mazishi ya mwanasiasa Mzee Jackson Kibor.

Marehemu atazikwa Aprili 1 nyumbani kwake karibu na Kabenes huko Uasin Gishu.

Kibor alifariki wiki jana akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuishi maisha ya umma yenye utata.

Familia ilisema kifo chake kilitokana na shambulio la Covid-19 ambalo lilidhoofisha mapafu yake na viungo vingine vya mwili.

Kulingana na matakwa yake, Kibor atazikwa karibu na mke wake wa kwanza Mama Mary.

Familia imekuwa ikikutana nyumbani kwake huko Eldoret kupanga hafla ya mazishi yake.

Mmoja wa wanawe Philip Kimutai alisema babake alitambua eneo lake la kuzikwa siku chache kabla ya kifo chake mnamo Machi 18.

"Mzee alikuwa ametuambia matakwa yake yote ikiwa ni pamoja na eneo la kaburi lake na tutazingatia hilo kikamilifu," Kimutai alisema.

Ingawa familia hiyo imetembelewa na watu wengi ikiwa ni pamoja na watu wa juu, walisema mzee aliwaambia wasitafute msaada wowote kwa mazishi yake.

Angalau fahali saba na mbuzi 50 watachinjwa kama sehemu ya sherehe za kumpeleka Mzee Jackson Kibor.

Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga na mkuu wa Kanu Gideon Moi ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria maziko hayo.

Hizi hapa baadhhi ya picha za matayarisho;

Image: Mathews Ndanyi
Image: Mathews Ndanyi
Image: Mathews Ndanyi
Image: Mathews Ndanyi