[Picha] Hafla ya mazishi ya hayati Mwai Kibaki yaendelea

Muhtasari

•Msafara wa mazishi ya Rais Mwai Kibaki umewasili katika uwanja wa Nyayo mwendo wa saa nne unusu asubuhi.

•Rais Uhuru Kenyatta  aliwasili katika uwanja wa Nyayo dakika chache kabla ya ibada ya mazishi ya Mwai Kibaki kung'oa nanga.

Marehemu Rais Mwai Kibaki akiwasili katika Uwanja wa Nyayo Aprili 29, 2022 kwa Ibada ya Mazishi ya Serikali.
Marehemu Rais Mwai Kibaki akiwasili katika Uwanja wa Nyayo Aprili 29, 2022 kwa Ibada ya Mazishi ya Serikali.
Image: ANDREW KASUKU

Msafara wa mazishi ya hayati  Mwai Kibaki umewasili katika uwanja wa Nyayo mwendo wa saa nne unusu asubuhi.

Jeneza linalosheheni mwili wa hayati lilikuwa limefungwa kwa bendera ya Kenya.Kikosi cha wanajeshi wa KDF kilikuwa kimezidikisha jeneza hilo.

Mwili wa Kibaki wawasili katika uwanja wa Jomo Kenyatta
Mwili wa Kibaki wawasili katika uwanja wa Jomo Kenyatta
Image: ANDREW KASUKU
Mwili wa hayati Mwai Kibaki wawasili katika uwanja wa Nyayo
Mwili wa hayati Mwai Kibaki wawasili katika uwanja wa Nyayo
Image: ANDREW KASUKU
Gwaride la kijeshi katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29,2022
Gwaride la kijeshi katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29,2022
Image: ENOS TECHE

Rais Uhuru Kenyatta  aliwasili katika uwanja wa Nyayo dakika chache kabla ya ibada ya mazishi ya Mwai Kibaki kung'oa nanga.

Rais alipokelewa na naibu wake William Ruto.

Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya mazishi ya hayati Mwai Kibaki
Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya mazishi ya hayati Mwai Kibaki
Image: EZEKIEL AMINGA
Rais Uhuru Kenyatta apokewa na naibu wake William Ruto
Rais Uhuru Kenyatta apokewa na naibu wake William Ruto
Image: EZEKIEL AMINGA

Zaidi ya viongozi 10 wa mataifa mbalimbali ni miongoni mwa wageni maalum ambao wamehudhuria hafla hiyo.