GRAFIKI: Pandashuka za Miguna Miguna kurejea Kenya

Miguna alifukuzwa nchini kwa mara ya kwanza mnamo Februari 6, 2018.

Muhtasari

•Kurejea kwa Miguna katika nchi yake ya kuzaliwa sasa kunaonekana kukaribia zaidi kuliko hapo awali.

Matukio ya Kufurushwa kwa Miguna
Image: SAMUEL MAINA NA WILLIAM WANYOIKE

Miguna Miguna sasa anaweza kutabasamu kwani kurejea kwake katika nchi yake ya kuzaliwa sasa kunaonekana kukaribia zaidi kuliko hapo awali.

Jumanne wakili huyo ambaye kwa sasa anaishi Kanada alitangaza kwamba ameweza kupokea pasipoti yake ya Kenya kwa maandalizi ya kurejea. Alibainisha kuwa aliweza stakabadhi hiyo muhimu iliweza kufikishwa kwake  kufuatia agizo la Rais William Ruto.

Mshauri huyo wa kisiasa wa zamani wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alidokeza kuwa atarejea nchini pindi tu baada ya vikwazo vilivyomzuia kuingia tena hapa nchini kuondolewa.

Miguna alifukuzwa nchini kwa mara ya kwanza mnamo Februari 6, 2018 baada ya kukamatwa na kuzuiliwa.Hii ni baada ya kuchukua hatua hatari ya kumuapisha Raila kuwa 'Rais wa Watu' kufuatia kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Alitakiwa kurejea nchini mwezi Novemba 2021 lakini hakuweza kutokana na vikwazo ambavyo viliwekwa dhidi yake.

Hapo awali alidokeza kuwa yupo tayari kurejea baada ya Ruto kutangazwa mshindi wa kinyang'anyiro cha urais.