Jinsi Kongamano la Wanaume la Kenya lilivyofanyika (+Picha)

Wanaume wa rika tofauti kutoka sehemu mbalimbali za nchi walihudhuria.

Muhtasari

•Hafla hiyo iliyofanyika katika Carnivore Simba Saloon ilianza saa nane mchana na kuendelea hadi baadaye jioni.

•Wanajopo walijumuisha aliyekuwa Jaji Ian Mbugua, wakili Danstan Omari, Dkt Frank Njenga, Mjumbe Robert Alai, Mhubiri Simon Mbevi na Chris Kirwa.

wakiwasili kwenye Carnivore Simba Saloon kwa ajili ya Kongamano la Wanaume 2023 siku ya Jumanne Februari 14.
Kikundi cha Wanaume wakiwasili kwenye Carnivore Simba Saloon kwa ajili ya Kongamano la Wanaume 2023 siku ya Jumanne Februari 14.
Image: WILFRED NYAGARESI

Kongamano halisi la kwanza kabisa la Wanaume kutokea nchini Kenya lilifanyika katika Carnivore Simba Saloon siku ya Jumanne alasiri.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Kongamano la Wanaume wa Kujitangaza Stephen Letoo ilianza saa nane mchana na kuendelea hadi baadaye jioni.

Wanaume wa rika tofauti kutoka sehemu mbalimbali za nchi walihudhuria hafla hiyo iliyopambwa na watu kadhaa mashuhuri nchini.

Mfawidhi wa tukio hilo lenye utata alikuwa mchekeshaji Dr Ofweneke pamoja na mtangazaji maarufu Shaffie Weru.

Wanajopo wa Toleo la Kenya la Kongamano la Wanaume la 2023 walijumuisha aliyekuwa Jaji wa Tusker Project Fame Ian Mbugua, wakili maarufu Danstan Omari, Mwanasaikolojia Dkt Frank Njenga, Mjumbe wa Kileleshwa Robert Alai, Mhubiri Simon Mbevi na Chris Kirwa.

Wageni wengine ni pamoja na mwanahabari mkongwe Swaleh Mdoe, kiongozi wa Wachache katika Kaunti ya Nairobi Mhe. Anthony Kiragu Karanja miongoni mwa wengine.

Miongoni mwa mada za siku hiyo ni Afya ya Akili ya Wanaume, Ndoa za wake wengi, Mahusiano, Masuala ya Uzazi Wenza, Talaka na Uzazi.

Tazama Picha la Hafla hiyo:-

mnamo Jumanne Februari 14.
Wanajopo wa Kongamano la Wanaume 2023 Dkt Frank Njenga, Mhubiri Simon Mbevi, Jaji Ian Mbugua na wakili Danstan Omari mnamo Jumanne Februari 14.
Image: WILFRED NYAGARESI
Waandalizi wa Kongamano la Wanaume wakiwemo Shaffie Weru na Stephen Letoo
Image: WILFRED NYAGARESI
wakiwasili kwenye Carnivore Simba Saloon kwa ajili ya Kongamano la Wanaume 2023 siku ya Jumanne Februari 14.
Kikundi cha Wanaume wakiwasili kwenye Carnivore Simba Saloon kwa ajili ya Kongamano la Wanaume 2023 siku ya Jumanne Februari 14.
Image: WILFRED NYAGARESI
akizungumza kwenye Kongamano la Wanaume 2023 lililofanyika Carnivore Simba Saloon siku ya Jumanne Februari 14.
Dkt Frank Njenga akizungumza kwenye Kongamano la Wanaume 2023 lililofanyika Carnivore Simba Saloon siku ya Jumanne Februari 14.
Image: WILFRED NYAGARESI