Waiguru:Kwa sasa, mpango wangu ni kutetea kiti changu cha ugavana

Muhtasari
  • Gavana Waiguru asema mpango wake ni kutetea kiti chake cha ugavana
Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi
Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi
Image: MAKTABA

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Ann Waiguru ametangaza kuwa atatetea kiti chake, alitupilia mbali madai kwamba amepanga kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Akiwahutubia waandishi wa habari siku ya JUmatano Waiguru amesema kwamba hajaketi na wawaniaji wa urais wa mwaka wa 2022 ili awe mwenzake katika kinyang'anyiro hicho.

Waiguru alisema kuwa hana shida na watu kutoka mkoa wa Mt Kenya  atakaye tangaza matakwa yao ya kufanikisha Kenyatta.

"Kwa sasa, mpango wangu ni kulinda kiti changu ... Hiyo ni mpango wangu mpaka kutakapokuwa na hoja tofauti Sijaketi na mtu yeyote kujadili swali la mwenzi   ," Waiguru alisema

Alisema kwamba mazungumzo ambayo yanaendelea kuwa atakuwa mwenzi wa mwaniaji urais sio jambo mbaya kwani ni heshima kwa wananchi wa KIrinyaga.

"Sio jambo baya. Inaonyesha kwamba watu wanakuamini. Ninaona kama heshima kwa watu wa Kirinyaga,"Waiguru Alizungumza.

Katika kesi ya Muturi, alisema Wakenya wote wana haki ya kuishi kwa nafasi ambazo zitakuwa za kunyakua katika uchaguzi.

"KIle tulikataa ni jinsi mtu alivyokuwa msemaji lakini sasa amebadilika tangu tunapomwona mtu anataka kuwa rais," Waiguru alisema.