UN yataka Uingereza kuomba msamaha na kufidia jamii za Magharibi mwa Kenya zilizodhulumiwa enzi za ukoloni

Uingereza imetakiwa kuomba msamaha na kuwalipa fidia watu kutoka jamii mbili za magharibi mwa Kenya ambao walinyanyaswa na ardhi zao zilichukuliwa enzi za ukoloni.

Muhtasari

•Umoja umesema kuwa watu wa jamii ya Kipsigis na Tailai communities na wengine wazawa walidhulumiwa na na kutendewa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji, dhulma za kingono, kudhalilishwa, kuwekwa kizuizini kiholela, kuhamishwa kiholela na kunyimwa haki za faragha, maisha ya familia na mali.

•Sehemu kubwa ya ardhi katika eneo hilo sasa inamilikiwa na Uingereza na makampuni makubwa yakimataifa ya chai ikiwemo Findlay’s, Williamson Fine Tea na Unilever.

Ungereza makampuni ya kimataifa ya chai sasa Inamilikisehemu kubwa ya ardhu magharibi mwa Kenya
Ungereza makampuni ya kimataifa ya chai sasa Inamilikisehemu kubwa ya ardhu magharibi mwa Kenya
Image: BBC

Ungereza imetakiwa kuomba msamaha na kuwalipa fidia watu kutoka jamii mbili za magharibi mwa Kenya ambao walinyanyaswa na ardhi zao zilichukuliwa enzi za ukoloni.

Ombi la Wakenya wazawa ambao walikuwa wamekaa katika maeneo yenye chai ya kaunti ya Kericho liliwasilishwa mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa (UN).

Umoja umesema kuwa watu wa jamii ya Kipsigis na Tailai communities na wengine wazawa walidhulumiwa na na kutendewa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji, dhulma za kingono, kudhalilishwa, kuwekwa kizuizini kiholela, kuhamishwa kiholela na kunyimwa haki za faragha, maisha ya familia na mali.

Karibu watu 500,000 walidhulumiwa .

Sehemu kubwa ya ardhi katika eneo hilo sasa inamilikiwa na Uingereza na makampuni makubwa yakimataifa ya chai ikiwemo Findlay’s, Williamson Fine Tea na Unilever.

UN ilikuwa imeandikia serikali ya Uingereza mwezi Mei na kusema itachapisha matokeo ya uchunguzi wake ndani ya siku 30.