Seneta Mithika Linturi ashtakiwa kwa tuhuma za jaribio la ubakaji

Kulingana na mwanamke huyo, mwanaume yule alipoingia kitandani hakusema neno lolote wakati aliendelea kumshika isivyofaa na kisha baadae wakalala.

Muhtasari

•Seneta wa Meru Mithika Linturi amekabiliwa na tuhuma za kuingia ndani ya chumba cha malazi kilichokuwa kimekodishwa wanandoa wawili na kujaribu kubaka mwanamke.

•Ilipofika mwendo wa saa tisa usiku akaskia mlango ukiwa unafunguliwa na kwa kuwa taa zilikuwa zimezimwa akadhani kuwa ni mumewe.

•Marafiki waliokuwa nao walifika kuchunguza tukio lile na wakamtambulisha mhusika kuwa seneta Mithika Linturi

Seneta wa Meru Mithika Linturi
Seneta wa Meru Mithika Linturi
Image: ENOS TECHE

Habari na Annette Wambulwa

Seneta wa Meru Mithika Linturi amekabiliwa na tuhuma za kuingia ndani ya chumba cha malazi kilichokuwa kimekodishwa wanandoa wawili na kujaribu kubaka mwanamke.

Linturi amefika mahakamani kujaribu kuzuia polisi kumkamata ama kumshtaki na hatia ya ubakaji na ukosefu wa adabu yanayohusishwa na tukio hilo.

Kulingana na ripoti za polisi, mwanamke mmoja alipiga ripoti kuwa alikuwa na mumewe na marafiki katika hoteli ya Maiyan Villas Resort Nanyuki mnamo Januari 29 mwakani na baadae akaelekea kwa chumba ambacho walikuwa wamelipia pamoja na mumewe ila akapata mlango ukiwa umefungwa kwani bwanake hakuwa amerejea.

Ilipofika mwendo wa saa tisa usiku akaskia mlango ukiwa unafunguliwa na kwa kuwa taa zilikuwa zimezimwa akadhani kuwa ni mumewe. 

Mwanamke huyo aliripoti kuwa aliyeingia chumbani alianza kumshika kwa namna isiyo ya kawaida. 

Hata hivyo kulingana na mwanamke huyo, mwanaume  yule alipoingia kitandani hakusema neno lolote wakati aliendelea kumshika isivyofaa na kisha baadae wakalala.

Alidai kuwa takriban nusu saa baadae aliskia mlango ukibishwa na akaenda kufungua. Alipatwa na hali ya kuchanganyikiwa alipoona mumewe akiwa amesimama pale mlangoni na kushindwa kwani alikuwa amelala na nani kitandani.

Mwanadada yule alipowasha taa waligundua kuwa aliyekuwa kitandani ni mgeni kwao na hapo mumewe akapandwa na hasira na akaanza kupiga kelele iliyowaamsha wengine katika hoteli hiyo.

Marafiki waliokuwa nao walifika kuchunguza tukio lile na wakamtambulisha mhusika kuwa seneta Mithika Linturi.

Ilibainika kuwa Linturi pia alikuwa amelipia chumba katika hoteli ile karibu na kile cha wanandoa hao. Hata hivyo haikueleweka kana kwamba mwanasiasa huyo alikosea chumba chake ana kuingia cha wenyewe ama ilikuwa vipi.

Mwanamke yule alidai kuwa Linturi alijitolea kusuluhisha tukio hilo nje ya mahakama kwa kuwalipa shilingi milioni moja ila baadae aliwaripoti kwa kile alisema ni ulafi.

Hapo wanandoa hao wakaamua kumripoti seneta yule na kosa la jaribio la ubakaji na ukosefu wa nidhamu.

Huenda Linturi akashtakiwa kwa tuhuma hizo iwapo DPP atapitisha mashtaka yanayomkabili.

Kupitia wakili wake Charles Mwongela, Linturi anataka mahakama kuzuia polisi kumkamata na kumshtaki na makosa hayo.

Linturi alisema kuwa waziri Fred Matiangi alipokuwa mbele ya kamati ya seneti alidai kuwa walikuwa na mpango  wa kumshtaki na kosa la jaribio la ubakaji kama mashtaka ya nyongezi dhidi yake  juu ya mashtaka ya kughushi yanayomkabili.

Linturi amedai kuwa tuhuma hizo hazikufichuliwa kwake mwezi Mei mwakani alipopata hati ya kuzuia esi ya kughushi dhidi yake kuendelea.

Amesema kuwa mashtaka hayo yamempata kwa mshangao.