Mama ya ndugu waliouawa Kitengela apokea usaidizi wa wataalamu wa saikolojia kupambana na majonzi

Habari za kuhofisha kuhusu mauaji ya wanawe Fred Mureithi (30) na Victor Mwangi (25) pamoja na wapwa wake mnamo Agosti 8 zilivunja moyo wake sana.

Muhtasari

•.Wanjiru alijipata katika hali ya mshutuko na hadi kupelekwa katika hospitali moja jijini London Uingereza ambako amekuwa akiishi tangu 2018.

•Wanjiru kwa sasa anapokea usaidizi wa wataalam wa kisaikolojia familia akifuata haki na kudai hatua ya haraka ichukuliwe dhidi ya waliotekeleza mauaji hayo.

Lucy Wanjiu akipokea vipimo vya kidaktari nyumbani kwake Syokimau Jumapili jioni
Lucy Wanjiu akipokea vipimo vya kidaktari nyumbani kwake Syokimau Jumapili jioni
Image: KURGAT MARINDANY

Lucy Wanjiru, mama ya ndugu wawili miongoni mwa vijana wanne wa familia moja waliopoteza maisha yao maeneo ya Kitengela baada ya kutuhumiwa kuwa wezi wa mifugo hakuwahi fikiria kuwa angewahi kuja kuzika watoto wake wa pekee.

Habari za kuhofisha kuhusu mauaji ya wanawe Fred Mureithi (30) na Victor Mwangi (25) pamoja na wapwa wake mnamo Agosti 8  zilivunja moyo wake sana.

Wanjiru alijipata katika hali ya mshutuko na hadi kupelekwa katika hospitali moja jijini London Uingereza ambako amekuwa akiishi tangu 2018.

Ndugu yake alisema kuwa matumaini ya dadake yalikuwa kwamba ilikuwa kesi ya makosa ya utambulisho na kuwa wanawe sio miongoni mwa wanne waliouliwa wakiwa pamoja na binamu wao Mike George, 29, na Nicholas Musa, 28,.

Alijua kuwa wanawe walikuwa wazima. Walipenda kusherehekea ushindi wa kila mmoja wao.

Ukweli ulimpata mama huyo wa wawili alipowasili nchini siku ya Jumapili na kulakiwa na wapendwa wake isipokuwa Mureithi na Mwangi.

"Alilia sana alipofika katika uwanja wa ndege, hatungeweza kumtuliza. Kwa kawaida wanawe wangekuja kumlaki" Ndugu ya Wanjiru, James Macharia alisema.

Wanjiru alikuwa amekaa Uingereza ili kuhakikisha wanawe waliishi katika hali njema hadi watakapokomaa kabisa. Hata hivyo aliporudi nchini alikumbwa na nyumba tupu na mradi uliosimama.

Wanjiru kwa sasa anapokea usaidizi wa wataalamu wa saikolojia huku familia ikiendelea kufuata haki na kudai hatua ya haraka ichukuliwe dhidi ya waliotekeleza mauaji hayo.

Alipofika nchini, Wanjiru alifanyiwa vipimo kadhaa vya kidaktari. Macharia alisema kuwa alilazimika kutafutia dadake usaidizi wa daktari.

"Alikuwa analia mara kwa mara, hakuwa anakula na hakuwa anafanya chochote. Kufiwa na wanawe kumemuweza kabisa" Alisema.

Macharia alisema kuwa kwa sasa familia inategemea usiadizi wa wataalamu wa kisaikolojia na kanisa yao ya t Mary ACK, Mlolongo.

(Utafsiri: Samuel Maina)