Makali ya Corona: Visa vipya 788 vyarekodiwa, Vifo 28 vyaripotiwa

Mtoto wa siku 14 na mkongwe wa miaka 110 ni miongoni mwa walioripotiwa kupatikana na virusi vya Corona hivi leo

Muhtasari

•Kufikia sasa Kenya imekuwa na visa 234,589 vya wagonjwa wa COVID-19 kutoka kwa vipimo 2,368,930 vilivyofanywa. 

•Kufikia sasa angalau watu 1,925,446 wameweza kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona huku 801,486 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imeripoti visa vipya 788 vya wagonjwa wa COVID-19 kutoka kwa sampuli ya watu 6, 690 ambao wameweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Idadi hiyo inaashiria kuwa asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 11.8%.

Mtoto wa siku 14 na mkongwe wa miaka 110 ni miongoni mwa walioripotiwa kupatikana na virusi vya Corona hivi leo.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukizi ikirekodi visa 163 ikifuatwa na Kiambu ambayo iliandikisha wagonjwa 96 huku Nakuru na Nyeri zikifuata na wagonjwa 73 na 40 mtawalia.

Kufikia sasa Kenya imekuwa na visa 234,589 vya wagonjwa wa COVID-19 kutoka kwa vipimo 2,368,930 vilivyofanywa. 

Habari njema ni kuwa watu 1,478 wameweza kupona, 1386 wakiponea manyumbani huku 92 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Hii inaashiria kuwa jumla ya wagonjwa 219,706 wameweza kupona maradhi hayo kufikia sasa.

Wagonjwa 7,442 wanendelea kuhudumiwa manyumbani huku wengine 1,959 wakiwa wamelazwa katika vituo mbalimbali vya afya  nchini. 162 kati yao wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Ya kuhofisha ni kwamba vifo 28 zaidi vimeripotiwa  na kufikisha jumla ya vifo kutokana na Corona nchini kuwa 4,694.

Chanjo ya Corona.

Kufikia sasa angalau watu 1,925,446 wameweza kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona huku 801,486 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.