Balozi wa Kenya ashtumiwa kwa uwindaji haramu wa wanyamapori nchini Namibia

Kenya ili piga marufuku uwindaji haramu mwaka 1977 ili kuhifadhi wanyamapori wake.

Balozi Benjamin Langat
Balozi Benjamin Langat
Image: TWITTER

Balozi wa Kenya nchini Namibia ameshambuliwa mtandaoni baada ya picha inayomuonesha akiwa karibu na swara aliyeuawa akiwa na bunduki mkononi kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Benjamin Langat, ambaye hajatoa tamko lolote kuhusu picha hiyo , ametuhumiwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twitter kwa kukiuka kujitolea kwa Kenya kwa uhifadhi wa wanyamapori licha ya kupata ruhusa ya kuwinda nchini Namibia::

Wengi walitoa maoni juu ya kejeli ya picha hiyo kwenye chapisho la Ikulu kuhusu rais akipongeza mashirika ya wanyama pori ya Kenya kwa juhudi zao za kupambana na uwindaji haramu- mtumiaji mmoja wa twitter alitoa wito wa balozi huyo kurejeshwa nyumba:

Kenya ili piga marufuku uwindaji haramu mwaka 1977 ili kuhifadhi wanyamapori wake.

Namibia inaruhusu uwindaji wanyamapori na kutumia fedha hizo kuhifadhi wanyama wanaokabiliwa na tisho la kuangamia