Mwakilishi wa wanawake Kakamega akemewa mitandaoni baada ya kubandika jina lake kwa nyumba ya matope aliyojengea mkazi

Chapisho lake halikupokewa vizuri na maelfu ya Wakenya mitanadoni ambao walifurika pale kutoa hisia zao mbalimbali.

Muhtasari

•Bi Muhanda alipakia picha ya nyumba mpya ya matope ambayo alikuwa amejengea mmoja wa mkazi wa kaunti ya Kakamega na kuandika jina lake ili kuashiria kuwa ulikuwa mradi wake.

•Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Muhanda aliambatanisha picha hizo na ujumbe "Hii inanitia msukumo, kubadilisha maisha ya watu wangu" 

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda
Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda
Image: FACEBOOK

Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Kakamega Bi Elsie Muhanda amekabiliwa na ghadhabu kubwa ya wanamitandao baada ya chapisho lake la hivi karibuni kwenye  mtandao wa Facebook.

Bi Muhanda alipakia picha ya nyumba mpya ya matope ambayo alikuwa amejengea mmoja wa mkazi wa kaunti ya Kakamega na kuandika jina lake ili kuashiria kuwa ulikuwa mradi wake.

Kando ya picha ya nyumba hiyo mpya mbunge huyo alipakia picha nyingine iliyoonyesha mjengo hafifu wa hapo awali ambao ulibomolewa ili amjengee mkazi huyo nyumba mpya.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Muhanda aliambatanisha picha hizo na ujumbe "Hii inanitia msukumo, kubadilisha maisha ya watu wangu" 

Hata hivyo chapisho lake halikupokewa vizuri na maelfu ya Wakenya mitanadoni ambao walifurika pale kutoa hisia zao mbalimbali.

Muhanda ambaye alichaguliwa kwa tiketi ya chama cha ODM alilazimika kufuta chapisho hilo baada ya kupokea upinzani mkubwa mitandaoni.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za Wanamitandao:-

@DrEvansRichard Its too wrong for Elsie Muhanda (MP for Kakamega county) to brand someone's house in the name of support or lifting people's lives. Awouro.

@KarakachaJr; Naming a house of a peasant after your you is an old fashioned politics. We peasants deserves respect or you leave as alone

Aisha Said: Kakamega Woman Representative Elsie Muhanda took branding to another level after writing her name on the house she had built for a needy resident.

@ElishaAbok What a joke!!🤔 you help the poor but you decide to brand the house with your name for popularity?......... Elsie Muhanda you won't be forgiven by God..