Wanafunzi wachoma bweni Narok baada ya wavulana kukatazwa kusherehekea pamoja na wasichana

Muhtasari

•Kizaazaa kilianza wakati usimamizi wa shule hiyo ulikataza wanafunzi wa kiume kufanya ushirika wa pamoja ili kusherehekea kununuliwa kwa vifaa mpya vya muziki vya Muungano wa Wakristo (CU) .

•Seneta Ole Kina alisema kwamba inasikitisha kuona vijana wadogo wakiumia kwa sababu ya vijana wachache wakubwa amba hawathamini masomo.

Bweni lililoteketezwa
Bweni lililoteketezwa
Image: KNA

Habari na Ann Salaton (KNA)

Wanafunzi katika shule ya upili ya Eor Ekule iliyo katika eneo la Narok Mashariki walichoma bweni moja wakati walikuwa 

Kulingana na kamanda wa polisi katika kaunti ya Narok John Kizito, kizaazaa kilianza wakati usimamizi wa shule hiyo ulikataza wanafunzi wa kiume kufanya ushirika wa pamoja ili kusherehekea kununuliwa kwa vifaa mpya vya muziki vya Muungano wa Wakristo (CU) .

Inaripotiwa kuwa ghasia zilianza mida ya usiku wa manane huku vijana wakianza kutupa mawe, kitendo ambacho kilifanya mwalimu mkuu Margaret Nguku kuwaita polisi.

Polisi walipowasili walipata bweni la Loita ambalo huwa na wanafunzi 200 likiwa limeteketezwa tayari. 

Wakati gari la kuzima moto liliwasili tayari bweni lile lilikuwa limeteketea kabisa na mali ya thamana isiyotambulika kuharibiwa. Hata hivyo hakuna yeyote aliyejeruhiwa.

Upande wa mabweni ya wavulana ulifungwa ili kupatia nafasi uchunguzi zaidi kufanyika .

Seneta wa Narok Ledama Ole Kina ni miongoni wa waliofika kwenye eneo la tukio usiku wa Jumapili na anashuku kuwa vijana wakubwa ndio walitekeleza kitendo hicho.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Ole Kina alisema kwamba inasikitisha kuona vijana wadogo wakiumia kwa sababu ya vijana wachache wakubwa amba hawathamini masomo.