(+Picha) Hali ya utulivu yarejea Laikipia, kufuatia mashambulio ya majambazi

Wakazi bado wanaelezea hofu juu ya usalama wao.

Muhtasari

•Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Fred Matiangi ametoa wito kwa watoto wote warejee shuleni katika eneo hilo, na amewahakikishia kupewa usalama wa ziada.

Bado Baadhi ya wakazi wa Laikipia wanahofia usalama wao,licha ya serikali kuwahakikishia kuwa itawalinda
Bado Baadhi ya wakazi wa Laikipia wanahofia usalama wao,licha ya serikali kuwahakikishia kuwa itawalinda
Image: BBC

Hali ya utulivu imerejea katika kaunti iliyokumbwa na ghasia ya Laikipia katika mkoa wa Rift Valley nchini Kenya wiki moja baada ya mashambulio yaliyowaacha makumi kadhaa ya watu wakiuawa.

Wakazi wa maeneo ya Laikipia wamekuwa wakikumbwa na mashambulio ya majambazi wanaowashambulia kwa bunduki na kujificha msituni, hali iliyoifanya serikali ya Kenya kutuma maafisa wa usalama, ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Wakazi bado wanaelezea hofu juu ya usalama wao.

Maafisa wa usalama wanaofanya ulinzi wa doria, wanaonekana wakiwasindikiza watoto shuleni licha ya kwamba wanafunzi wengi walishindwa kuhudhuria masomo kama ilivyotarajiwa.

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Fred Matiangi ametoa wito kwa watoto wote warejee shuleni katika eneo hilo, na amewahakikishia kupewa usalama wa ziada.

Zifuatazo ni picha zinazoonyesha hali ilivyo katika eneo la Kisii Ndogo katika Kaunti ya Laikipia , ambako majambazi wamekuwa wakiwashambulia wakulima wadogo, kuchoma nyumba na kuiba mali.

Kaunti ya Laikipia , ambako majambazi wamekuwa wakiwashambulia wakulima wadogo, kuchoma nyumba na kuiba mali.
Kaunti ya Laikipia , ambako majambazi wamekuwa wakiwashambulia wakulima wadogo, kuchoma nyumba na kuiba mali.
Image: BBC
aadhi ya wakazi wa Laikipia wamepoteza makazi yao kufuatia mashambulio ya majambaz
aadhi ya wakazi wa Laikipia wamepoteza makazi yao kufuatia mashambulio ya majambaz
Image: BBC
Vikosi vya usalama vimepelekwa Laikipia kukabiliana na majambazi
Vikosi vya usalama vimepelekwa Laikipia kukabiliana na majambazi
Image: BBC
Vikosi vya usalama vimekuwa vikifanya ulinzi wa doria katika maeneo ya Laikipia ili kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi
Vikosi vya usalama vimekuwa vikifanya ulinzi wa doria katika maeneo ya Laikipia ili kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi
Image: BBC