Daktari adunga watoto wake wawili sindano yenye sumu kisha kujaribu kujitoa uhai Nakuru

Muhtasari

•Dawa za aina tofauti sirinji zilizokuwa zimetumika na kisu chenye makali ni baadhi ya vitu ambazo zilipatikana kwenye eneo la tukio.

crime scene
crime scene

Daktari mmoja anayefanya kazi mjini Nakuru anadaiwa kuwaua wanawe wawili kisha kujaribu kujitoa uhai usiku wa Jumamosi.

James Muriithi Gakara ambaye ni daktari wa uzazi katika hospitali ya Optimum Current Nakuru anaaminika kuwadunga watoto wake wenye umri wa miaka 5 na 3 na sindano iliyo na sumu ambayo iliwaua papo hapo.

Wapelelezi waliokuwa wamealikwa na majirani kuchunguza mbona daktari yule alikuwa amejifungia kwa nyumba pamoja na watoto wake, jambo lisilo la kawaida walipata miili ya watoto hao ikiwa imelala kitandani huku povu ikichemka midomoni.

Mshukiwa pia alipatikana akiwa amelala kitandani chake akiwa na povu mdomoni ila hakuwa amekata roho. Alikimbizwa katika hospitali ya Nakuru ambapo madaktari walinusuru maisha yake.

Dawa za aina tofauti sirinji zilizokuwa zimetumika na kisu chenye makali ni baadhi ya vitu ambazo zilipatikana kwenye eneo la tukio.

Kwa sasa mshukiwa anaendelea kupata nafuu hospitalini huku akisubiri kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la kuhofisha.