DCI watoa zawadi ya milioni 60 kwa atakayetoa habari ya washukiwa 3 wa Ugaidi Waliotoroka Gereza la Kamiti

Muhtasari
  • DCI watoa aawadi ya milioni 60 kwa atakaye toa habari ya washukiwa 3 wa Ugaidi Waliotoroka Gereza la Kamiti
Kamiti Max
Kamiti Max

Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imeanzisha msako wa kuwasaka washukiwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika Gereza la Kamiti Maximum saa za Jumatatu asubuhi.

Polisi walisema Musharaf Abdalla Akhulunga almaarufu Zarkawi/Alex/Shukri, Mohamed Ali Abikar na Joseph Juma Odhiambo almaarufu Yusuf walitoroka katika kituo cha kurekebishia tabia chenye ulinzi mkali mwendo wa saa moja asubuhi.

Katika notisi iliyosambazwa kwa umma kwenye Twitter, mkuu wa DCI George Kinoti alitoa zawadi ya Sh60 milioni kwa mtu yeyote aliye na habari ambazo zinaweza kusababisha kukamatwa kwa watatu hao. Polisi waliweka fadhila ya Sh20 milioni juu ya kichwa cha kila mshukiwa.

Musharaf alikamatwa mnamo Septemba 30, 2012, kwa kuhusika kwake katika jaribio lililoshindwa la kutekeleza shambulio la kigaidi lililolenga Majengo ya Bunge.

Alishtakiwa kwa kupatikana na vilipuzi, risasi na bunduki.

Mshukiwa anatoka eneo la Ekero huko Mumias ndani ya Kaunti ya Kakamega.

"Huduma ya Kitaifa ya Polisi inawafahamisha umma kwamba Musharaf ni hatari na inaomba taarifa zozote kuhusu aliko. Taarifa inaweza kushirikiwa kwa Fichua kwa DCI, piga simu ya simu ya bure 0800722203 ili kuripoti bila kujulikana. Usiogope! Zawadi: Ksh20,000,000,” alisema Kinoti.

Mohamed alikamatwa kufuatia kuhusika kwake na shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa lililotokea Aprili 2, 2015. Kinoti alisema Joseph alikamatwa mnamo Novemba 21, 2019 huko Bulla Hawa, Somalia alipokuwa akijaribu kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Joseph juma adhiambo Anatoka eneo la Lukoye, huko Mumia ndani ya Kaunti ya Kakamega.