Msitufungie jameni! Uhuru asihi mataifa ya kigeni juu ya aina mpya ya corona Omicron

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa mataifa ya kigeni kutofunga mipaka yao kutokana na aina mpya ya corona Omicron
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa mataifa ya kigeni kutofunga mipaka yao kutokana na aina mpya ya corona Omicron.

Akizungumza katika Bunge siku ya Jumanne, Uhuru alisihi kwamba mipaka hiyo iwachwe wazi.

"Usifunge wapanda. Msitufungie tena jameni ..Hakuna mtu ambaye ako salama  na Covid, hadi tutakapokuwa salama sote

"Covid-19 haitashindwa kwa kufunga nchi  au kwa kufunga sehemu za ulimwengu ambazo tunadhani zina shida,"Alisema.

Angola imekuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika kusimamisha safari za ndege kutoka kwa majirani zake wa eneo katika jitihada za kuzuia kuenea kwa aina mpya ya corona Omicron ya virusi vya corona, shirika lake la ndege la kitaifa lilisema.

Orodha ndefu ya nchi zimefunga mipaka yao kwa eneo hilo tangu wanasayansi wa Afrika Kusini kutangaza aina  mpya ya coronavirus wiki iliyopita.

Kusimamishwa ni kwa kuzingatia uamuzi wa serikali wa kupiga marufuku kwa muda mawasiliano ya anga kwenda Botswana, Eswatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe, ilisema katika taarifa.

Wakati huo huo aliwasihi wakenya kupokea chanjo ya corona ili kupigana na aina mpya ya corona Omicron.