Raila amteua Gavana wa Laikipia Nderitu Murithi kama mwenyekiti wa kampeni zake za urais

Muhtasari
  • Elizabeth Meyo ameteuliwa kuhudumu kama mtendaji mkuu wa bodi hiyo
  • Bodi hiyo itakuwa injini ya kampeni ya urais ya aliyekuwa waziri mkuu ambayo itaendesha azma yake ya kumrithi Rais Uhuru Kenyatta
Gavana wa kaunti ya Laikipia Ndderitu Murithi
Image: Maktaba

Gavana wa Laikipia Nderitu Murithi ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya kampeni za urais za kinara wa ODM Raila Odinga.

Elizabeth Meyo ameteuliwa kuhudumu kama mtendaji mkuu wa bodi hiyo.

Bodi hiyo itakuwa injini ya kampeni ya urais ya aliyekuwa waziri mkuu ambayo itaendesha azma yake ya kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Murithi ambaye anahudumu muhula wake wa kwanza ni mwanauchumi wa zamani wa benki ya dunia na masoko ya fedha, mtaalamu.

Yeye ndiye mwenyekiti wa sasa wa kamati ya fedha, mipango na masuala ya uchumi wa Baraza la Magavana aliyechaguliwa Januari 2021.

Alipochaguliwa kuwa Gavana wa Laikipia mnamo 2017, Muriithi alianza mageuzi makubwa ya utumishi wa umma wa kaunti ili kuifanya iwe ya kitaalamu na ya ushindani duniani.

“Gavana wa Laikipia, H.E. Mhe Ndiritu Muriithi, ameteuliwa na kukubaliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Kampeni ya Raila Odinga 2022,” alisema Raila kwenye taarifa yake Januari 5, 2022.

Meyo, ambaye kwa sasa ni mshauri wa IMF, atakuwa afisa mkuu mtendaji wa sekretarieti na ataleta tajriba ya kiutawala na kimkakati kwa zaidi ya miongo mitatu kwenye nafasi hiyo.

Yeye ni Kamishna wa zamani wa Idara ya Ushuru wa Ndani katika Mamlaka ya Ushuru ya Kenya. Wakati wa utumishi wake katika KRA.

Meyo atakuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampeni, kutekeleza maamuzi yake ya kimkakati na muhimu, mkuu wa sekretarieti ya kampeni, na kufanya maamuzi yote muhimu. Atakuwa msemaji pekee wa kampeni.