Niliachia Raila, Kalonzo kwa maana niliona hapendi Mungu-DP Ruto adai

Muhtasari
  • DP William Ruto amemsuta kiongozi wa Wiper Kalonzo kwa kumuunga mkono kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kuwania urais
Naibu Rais William Ruto akihitubia wakazi wa Kangundo kaunti ya Machakos Alhamisi Januari 20/2022
Image: Geroge Owiti

DP William Ruto amemsuta kiongozi wa Wiper Kalonzo kwa kumuunga mkono kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kuwania urais.

"Mimi sina shida na mtu yeyote, nilisaida Raila hadi akawa Prime Minister lakini ilifika wakati nikagundua hapendi Mungu nikachoka nikamwachia Kalonzo

Kalonzo alimsukuma hadi siku hizi nywele yake imekwisha. Ukipata mtu analalamika juu ya Kanisa, jua kuna shida," Ruto alisema.

Ruto alidai kuwa Raila hawezi kushinikizwa kuwa rais zaidi.

"Niko hapa ili yeye(Raila) asije kukusumbua," alisema huku akicheka.

Ruto zaidi alimwambia Raila aepuke ghasia kabla ya uchaguzi wa Agosti 9.Aliwataka washindani wake kutoendelea kutoa visingizio kuhusu vurugu.

"Ninataka kuwahimiza washindani wangu kuhakikisha kuwa katika mlingano wetu wa uchaguzi hakuna vurugu," Ruto alisema.