Huzuni!Watoto wa wanandoa waliofariki siku ya Krismasi wakwama hospitalini

Muhtasari
  • Watoto wa wanandoa waliofariki siku ya Krismasi wakwama hospitalini
  • Hii imefanya iwe vigumu kwao kupata nyumba na hata kupata nguo za ziada kwa ajili ya watoto
Image: Hisani

Watoto wawili walioachwa baada ya wazazi wao Ronald na Veronica Bundi kufariki katika ajali ya gari mkesha wa mkesha wa Krismasi sasa wamekwama hospitalini.

Akiongea wakati wa mahojiano na runinga ya Citizen, dadake marehemu Veronica anasema kakake marehemu Ronald Bundi ameifungia familia hiyo nyumba.

Hii imefanya iwe vigumu kwao kupata nyumba na hata kupata nguo za ziada kwa ajili ya watoto.

"Watoto hao waliruhusiwa kuondoka wiki iliyopita lakini bado wako hospitalini. Shida ni kwamba mjomba wao (kaka kwa marehemu baba yao) ametunyima kupata nyumba. Hatuwezi hata kuingia ili kuwachukulia watoto nguo za kubadili,” alisema dada mmoja kwa Marehemu Veronicah.

Kulingana na walioshuhudia, Ronald, ambaye alikuwa akiendesha gari, alikufa papo hapo pamoja na binti zake wawili, Natalia, 14, na Clare, 7. V

eronicah alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu siku tatu baadaye huku Marion, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Star of the Sea, Mombasa, akifariki dunia Desemba 31.

Wana wao wawili wa kiume wenye umri wa miaka 10 na 3, walipata majeraha mabaya na kukimbizwa katika hospitali moja mjini Voi kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali Kuu ya Pwani.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, watoto wawili walioachwa wamekwama katika hospitali ya Coast General kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Mnamo Januari 7, 2022, marehemu Bundi, mkewe Veronicah na watoto wao watatu walizikwa nyumbani kwao katika Kaunti ya Kisii; lakini kwa watoto wawili ambao bado walikuwa wakiuguza majeraha hospitalini, huu ulikuwa mwanzo wa changamoto zilizochochewa kwa kiasi kikubwa na mzozo wa mali za wazazi wao.