DP Ruto anafaa kumchagua mwanamke kutoka mlima Kenya kama mgombea mwenza-Ann Waiguru

Muhtasari
  • Gavana huyo alisema ingawa Ruto ana jukumu la pekee la kumchagua mgombea mwenza, angefurahi kumchagua
  • Hata hivyo, gavana huyo alisema ataheshimu chaguo la Ruto la mgombea mwenza
waiguruwithnewhairdo
waiguruwithnewhairdo

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amemtaka Naibu rais William Ruto kumchagua mgombea mwenza mwanamke kutoka eneo la Mlima Kenya.

Waiguru alisema "anatumai Ruto atamchagua mgombea mwenza wake kutoka eneo la Mlima Kenya kwa sababu eneo hilo lina idadi kubwa ya kura za kumpitisha kwenye Urais.

Gavana huyo alisema ingawa Ruto ana jukumu la pekee la kumchagua mgombea mwenza, angefurahi kumchagua.

"Ninachojua mimi uamuzi wa nani atakuwa mgombea mwenza ni uamuzi wa William Ruto. Kitu pekee tunachotarajia ni suala la wapi anatoka mgombea mwenza. Mjadala ni kwamba mtu huyo atoke mkoa wa mlima Kenya,” Waiguru alisema.

Alikariri kuwa siasa ni mchezo wa nambari UDA ilikuwa na matumaini ya kushinda uchaguzi wa 2022.

Alisema DP Ruto anafaa zaidi kumrithi Rais Uhuru Kenyatta kwa vile anaelewa vyema, maendeleo yanayoendelea yanafanya kazi.

Waiguru ni miongoni mwa viongozi ambao majina yao yameonekana maarufu miongoni mwa wawaniaji mwenza wa wagombea urais.

"Nadhani itakuwa heshima kubwa kuchaguliwa kama mgombea mwenza wa UDA, lakini hivi sasa juhudi zangu zote ni kutetea kiti changu cha ugavana wa Kirinyaga," aliongeza.

Hata hivyo, gavana huyo alisema ataheshimu chaguo la Ruto la mgombea mwenza.

Waiguru ambaye alizungumza wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha redio, alisema UDA imeanzisha mipango kadhaa ya kimakusudi kusaidia kuziba pengo la kijinsia katika uwakilishi kwa kuhimiza wanawake zaidi kuwania viti vya kisiasa.

Aidha gavana huyo alisema uamuzi wake wa kujiunga na UDA uliarifiwa na wapiga kura wa Kirinyaga.

"Wananchi wa Kirinyaga walisema wameridhishwa na kazi ya maendeleo tuliyofanya, hata hivyo walisema hawatanichagua tena isipokuwa nijiunge na UDA," alisema.

Waiguru aliongeza kuwa UDA ndicho chama maarufu zaidi cha kisiasa katika Mlima Kenya na yeyote anayesema vinginevyo anajidanganya.

"Nimesikiliza hoja na ni wazi kuwa chama ni UDA na mgombea wao wa Urais ni William Ruto."