Jahmby Koikai kuwania ubunge wa Dagoretti Kusini katika uchaguzi ujao

Muhtasari
  • Jahmby ameweka wazi kwama atakuwa mgombea binafsi ambaye atawania kiti cha ubunge wa Dagoretti
  • Kiini kikuu cha Jahmby kujiunga na siasa ni kwamba anataka kubadilidisha maisha ya vijana na akina mama
Kila siku zake zilipokaribia, alikuwa anapatwa na uchungu mwingi. Picha; JAHMBY KOIKAI.
Kila siku zake zilipokaribia, alikuwa anapatwa na uchungu mwingi. Picha; JAHMBY KOIKAI.

Jahmby Koikai kupitia kwenye ukurasa wake ametangaza kwamba anajitosa kwenye ulingo wa siasa katika uchaguzi mkuu ujao Agosti 9.

Jahmby ameweka wazi kwama atakuwa mgombea binafsi ambaye atawania kiti cha ubunge wa Dagoretti.

Kiini kikuu cha Jahmby kujiunga na siasa ni kwamba anataka kubadilidisha maisha ya vijana na akina mama, na kuwapa wakazi wa Dagoretti maisha mema

Pia alisema kwama anataka kuboresha afya na maji katika eneo hilo.

Huku akizungumzia hayo alikuwa na haya ya kusema;

"Naitwa Mary Njambi Koikai. Nilizaliwa na kukulia Dagoretti, Nairobi na mama mmoja na nyanya yangu na jamii inayotuzunguka

Kama wengine wengi, familia yangu ilijidhabihu ili kulipia elimu yangu. Nilihudhuria shule Nairobi kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu

Walitaka niwe na njia ya kutoka katika umaskini na maisha bora ya baadaye. Nilikua Dagoretti, nilipitia hali ngumu ya maisha katika jamii yetu kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali

Roho ya jumuiya na huduma kwa wengine iliingizwa ndani yangu nikiwa na umri mdogo kwa sababu tulilazimika kutunzana kama familia, majirani na marafiki."

Aliongeza na kusema;

 

"Tumekumbana na changamoto nyingi kama jumuiya kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya, usalama duni na huduma za kimsingi. Watu katika Dagoretti Kusini wanatamani kuishi maisha bora kwa ajili yao na watoto wao.

Roho ya jumuiya na kusudi inaweza kuonekana katika harakati zetu, urafiki ambao tumeunda tangu utotoni ambao umepitishwa kutoka kizazi hadi kizazi

Kuishi katika jamii hii kumeunda maadili yangu na mwelekeo wa maisha yangu. Hili limenitia moyo kufanya kazi kwa ajili ya jumuiya yangu ili kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi ya watu wetu kwa kufanya kazi pamoja,"Jahmby Aliongeza.