Mwanamke aliyeibiwa figo kazini Saudia alilia haki

Muhtasari

• Judithi aliyeondoka Uganda kuelekea Saudia kwa kazi za nyumbani aliibiwa figo yake wakati mwajiri wake alimshrutisha kumpeleka hospitali kwa chanjo ya Corona

• Katika harakati za kuchanjwa, alipoteza fahamu na alipogutuka akapata ako na kidonda tumboni ambapo hakuna aliyemjibu alipotaka kujua kiini cha kidonda hicho cha upasuaji

Judith Nakintu
Image: Nixon Praise (Facebook)

Mwisho wa mwezi Januari, habari za kusikitiza za kuibwa kwa figo ya mwanamke mmoja kutokea nchini Uganda aliyekuwa mfanyakazi wa ndani nchini Saudi Arabia zilizagaa mitandaoni huku wengi wakikashfu unyama wa mwajiri wake Mwarabu.

Mwanamke huyo, Judith Nakithu aliondoka nchini Uganda mwezi Desemba mwaka 2019 kuelekea Saudi Arabia kwa kazi ya ndani ambapo inaarifiwa siku za mwanzo mwanzo alikuwa akiwasiliana na familia yake nchini Uganda kupitia kwa simu ila mawasiliano haya yalikatishwa baada ya muda wa wiki mbili.

Katika mahojiano ya kipekee na runinga moja nchini humo, ndugu zake walieleza jinsi waliingiwa na wasiwasi baada ya mawasiliano kukatika ghafla na hapo ndipo walikumbuka Judith alikuwa amewaandikia namba ya bosi wake nchini Saudia ambapo juhudi zote za kumfikia ili wajue mwanao anaendelea vipi ziligonga mwamba.

Ndugu yake Robert Kadichi hakufa moyo na aliendelea kumtafuta bosi wake ambapo baadae Mwarabu huyo aliwaambia kwamba Judith alipata ajali mbaya iliyomlazimu kulazwa hospitali. Familia hiyo haikushawishiwa na taarifa hizi za bosi wa Judith ambapo walimtaka awatumie picha za mwanao akiwa hospitalini, lakini bosi huyo alikataa katakata na mwisho wa siku akawablock kwenye mtandao wa WhatsApp.

Baada ya juhudi zote hizi kugonga mwamba, walibakia na risasi moja tu katika bunduki zao, nalo lilikuwa ni kumtafuta wakala wa kampuni ambayo ilimtafutia kazi mwanao. Lakini pia wakala huyo alizidi kuwapigisha michezo ya paka na panya ambapo aliwaambia wawe na Subira kwani mwanao yuko hospitalini na alikuwa anapokea matibabu.

Pindi siku zilizidi kuzaa miezi na miezi ikatundika miaka, Judith alisafirishwa kurudi nchini kwao Uganda mwishoni mwa mwaka 2021, baada ya Zaidi ya mwaka mmoja bila kuwa na mawasiliano na watu wa nyumbani, huku wasiwasi ukiwa umetanda kuhusu afya yake.

Hapo ndipo Judith alimwaya mtama na kueleza kinagaubaga yaliyomsibu akiwa Uarabuni. Mwanamke aliyeibiwa figo kazini Saudia alilia haki na baadae alipopata fahamu, alipata ako na kidonda cha upasuaji katika tumbo lake na alipouliza nini kimemtokea mpaka akafanyiwa upasuaji, kila mtu alimtumbulia macho, pasi na wa kumpa maelezo.

“Wakati nilihisi uchungu, niliinua nguo na kuona kidonda tumboni. Nilipouliza nini kimetokea hakuna aliyenipa jibu,” alieleza Judith

Familia yake ilipigwa na butwaa na kuhakikisha mwanao anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu ili kubaini kama kweli ana viungo vyote vya ndani.

Vipimo vya CT-Scan na Xray vya mara ya kwanza katika hospitali ya Mulago nchini Ugandqa vilionesha kwamba Judith alikuwa na viungo vyote vya ndani ila familia bado haikushawishika na kutaka uchunguzi mwingine kufanywa ten ana tena.

Baada ya uchunguzi wa vipimo vya ndani ya mwili, ilibainika kwamba Judith hakuwa na figo yake ya kulia ambayo sasa imeulemaza upande wa wa kulia wa mwili wote na sasa hawezi tena kutembea saw ana huwa anatetemeka kw asana.

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo ilithibitisha hilo baada ya kupewa ripoti ya uchunguzi kutoka Hospitali kuu ya kitaifa ya Mulago na uchunguzi wa awali wa Polisi ulitambua mwajiri wake wa nchini Saudi Arabia kwa jina la Sadaffa Muhamed na kusema kwamba alitoa ripoti bandia za kitabibu kuwadanganya wanafamilia ya muathiriwa. Polisi walihakikishia familia hiyo kwamba haki itatendeka kwa mwanao Judith