(Picha+Video) Mwanamke ajinyonga Saudia kwa kunyimwa nafasi ya kuona mtoto wake na mumewe aliyehitaji 10K

Muhtasari

• "Ile harakati ya kuongea anahitaji mtoto wake, wakamuomba elfu kumi na yeye alisema ako na elfu tano lakini wakakataa na ndio maana akaamua kujinyonga,” - Ajenti

Mwanadada Eunice aliyejinyonga huko Saudia
Mwanadada Eunice aliyejinyonga huko Saudia
Image: Bro Dennis Onyamo//Facebook

Mwanamke mmoja anadaiwa kujitia kitanzi akiwa kazini huko Saudia Arabia kutokana na kile familia ilisema ni kukorofishana na mumewe ambayo yumo humu nchini kwa kukataa mwanamke huyo kuona mtoto wake.

Mwanadada huyo aliyetambulika kwa jina Eunice kutoka kaunti ya Kisii alifikia uamuzi wa kukatisha uhai wake pale alipodaiwqa shilingi elfu kumi na mumewe ili kuuona mtoto wake ambaye alimuacha naye kabla ya mume huyo kuoa mke mwingine tena, pale Eunice aliposafiri kuelekea taifa hilo la Milki za Kiarabu kwa ajili ya kazi.

“Alijiuwa Uarabuni baada ya kufuatilia bwana yake ameoa na mtoto alikuwa kwqa mzee wake huyo. Ile harakati ya kuongea anahitaji mtoto wake, wakamuomba elfu kumi na yeye alisema ako na elfu tano lakini wakakataa na ndio maana akaamua kujinyonga,” alisema kwa simu wakala ambaye alimpeleka dadake Marehemu kufanya kazi pia katika Milki za Kiarabu.