Genge la Majambazi lililonaswa kwenye CCTV likiwahangaisha wakazi wa Mombasa lakamatwa

Muhtasari
  • Genge la Majambazi lililonaswa kwenye CCTV likiwahangaisha wakazi wa Mombasa lakamatwa
Pingu
Image: Radio Jambo

Siku mbili baada ya genge la wahaifu lililonaswa kwenye kamera za CCTV likiwahangaisha wakazi wa Old Town kaunti ya Mombasa hatimaye wamekamatwa.

Kulingana na kurugenzi ya makosa ya Jinai DCI, kupitia kwenye ukurasa wa twitter genge hilo, lili naswa likitekeleza uhalifu huo, na lina majambazi 15.

Watano hao walikamatwa siku ya Ijumaa.

Kanda ya video ya vijana hao 15 ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha baadhi ya Wakenya  kudai wachukuliwe hatua.

Katika video hiyo, kikundi hicho kinaonekana kuwashambulia wanaume wawili ambao walikuwa wakifanya biashara zao mnamo Aprili 19, 2022.

Kufuatia kisa hicho, kundi la maafisa waliotoka katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mombasa, wakiungwa mkono na maafisa wa DCI wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) walianzisha operesheni ya kuwakamata washukiwa hao.

Washukiwa watano wa majambazi walionaswa kwenye picha hiyo walikamatwa kando katika maeneo ya Kibokoni, Kikowani na Makadara katika mji wa Mombasa.

Washukiwa hao ni pamoja na Noordin Mohamed, Brian Ogutu, Vidich Nzilu, Ahmed Ali na Abdala Mohamed.

Maafisa wa upelelezi wamebaini kuwa watano hao ni wa kikosi maarufu kilichoundwa hivi majuzi kinachojulikana kama genge la 'Haipingwi',

"Wapelelezi wa siri kutoka kwa timu za DCI sasa wako kwenye dhamira ya kuliangamiza kabisa genge la 'Haipingwi'," DCI ilisema.

Huku hayo yakijiri, majambazi waliosalia ambao bado wako huru wameonywa ama kujisalimisha au kukumbwa na hali sawa na iliyokumba genge la Mathare almaarufu Katombi.