Boniface Mwangi atafuta Picha za watu 2 Walioiba Ksh 18M kutoka kwa mteja

Muhtasari
  • Boniface Mwangi atafuta Picha za watu 2 Walioiba Ksh 18M kutoka kwa mteja
Mwanaharakati Boniface Mwangi
Image: Hisani

Boniface Mwangi ambaye ni miongoni mwa watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya leo kupitia kwenye  ukurasa wake wa twitter alisema  kuwa natafuta picha za Grace Kiptui na James Kipkemei, washirika wa Kiptui,Mawakili wa Kipkemei & Associates.

Mwangi alisema anafanyia kazi habari ya jinsi walivyoiba Kshs 18 milioni kutoka kwa mteja na @lawsocietykenya & @DCI_Kenya wakawalinda.

"Natafuta picha za Grace Kiptui na James Kipkemei, washirika wa Kiptui Kipkemei & Associates Advocates. Ninashughulikia hadithi ya jinsi walivyoiba Kshs milioni 18 kutoka kwa mteja na @lawsocietykenya

& @DCI_Kenya kuwalinda. Tutarekebisha Kenya mtu mmoja mmoja."

Ni ujumbe ambao ulibua hisia tofauti miongoni mwa wakenya huku wengi wakieleza jinsi kumekuwa na mawakili wa uongo nchini.