(+PICHA)Tazama jinsi basi la Guardian lilivyoteketea kwa moto

Muhtasari
  • Tazama jinsi basi la Guardian lilipoteketea kwa moto
Basi la Guardian lililoteketea kwa moto
Image: DANIEL ONGENDO

Zaidi ya abiria 40 walinusurika bila majeraha baada ya basi la Guardian Angel walimokuwa wakisafiria kushika moto katika eneo la Buoye kwenye barabara ya Ahero-Kisumu siku ya Jumatatu.

Basi hilo lilikuwa likielekea Nairobi kutoka Busia wakati kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 5.45 asubuhi.

Sababu ya moto huo haijabainishwa.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kisumu Alphonce Kimathi alisema basi hilo lilikuwa limebeba abiria 45 na hakuna majeruhi walioripotiwa.

Hizi hapa baadhi ya pcha za tukio hilo;

Image: DANIEL ONGENDO
Image: DANIEL ONGENDO
Image: DANIEL ONGENDO
Image: DANIEL ONGENDO