Naomba mnisamehe,'Anne Wamuratha avunja kimya baada ya video akigawa keki kuzua mtafaruku

Muhtasari
  • Anne Wamuratha avunja kimya baada ya video akigawa keki kuzua mtafaruku
  • Wamuratha alionekana akitumia mikono yake na kutupa keki huku na huko kana kwamba analisha kuku

Anne Wamuratha amekuwa akivuma katika mitandao ya kijamii kwa sababu zisizo sahihi katika siku chache zilizopita.

Katika video hiyo, mgombea uwakilishi wa wanawake Kiambu Anne wamuratha alionekana akiwagawia wakazi keki kwa njia ambayo imewaacha wengi wakiwa na hasira.

Wamuratha alionekana akitumia mikono yake na kutupa keki huku na huko kana kwamba analisha kuku.

Baada ya kukashifiwa na wanamtandao kwa matendo yake, mgombea huyo maarufu wa uwakilishi wa wanawake ameomba msamaha.

Katika chapisho lake la tarehe 4 Mei, Wamuratha ameomba msamaha wa dhati kwa wakazi wa Kiambu akifichua kuwa video hiyo ni ya mwaka wa 2021.

Wamuratha amesema kama angerudisha wakati nyuma, atafanya kila kitu tofauti na kilichotokea katika uwanja wa Ruiru.

Hapo awali, mshindani wake Loise kim alikuwa ameomba msamaha kwa umma kwa hatua ya Wamuratha.

Cha kusikitisha ni kwamba alishambuliwa na watumiaji wa mtandao kwa kutumia kuanguka chini kwa Wamuratha kwa manufaa yake.

"Anne Wamuratha, Mgombea Uwakilishi wa Kike wa Kiambu Aomba Radhi kwa Matukio ya Keki Ningependa kuthibitisha kuwa mimi ndiye niliyenaswa katika Video nikirusha vipande vya keki kwa kikundi cha watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Ruiru kwa hafla ya Novemba 7, 2021.

Nilikuwa msimamizi wa keki wa siku hiyo na nilikosea. kudhibiti umati na kushiriki keki ipasavyo. Ninaomba radhi kwa kitendo hicho kwa undani na kwa dhati na ninaomba wananchi wanisamehe. Ikiwa ningerudisha saa nyuma, ningesambaza keki tofauti.

Mimi ni mama na mke nimeazimia kuoka keki kubwa zaidi ya fursa kwa wakazi wa Kiambu na kuwahudumia kwa bidii kama mwakilishi wao wa wanawake

Kwa mara nyingine tena, ninaomba msamaha kwa dhati na kukubali kosa langu, halitatokea tena. Wako wa kweli, Anne Wamuratha," Aliandika Anne.