'Kama hakuheshimu hastahili kura yako,'Charity Ngilu awaambia wanawake huku akimlipua Gachagua

Muhtasari
  • Baadhi ya viongozi kutoka muungano wa Kenya Kwanza walimshambulia Karua
Gavana wa Kitui Charity Ngilu
Image: Musembi Nzengu

Baada ya muungano wa Azimio kumtambulisha mgombea mwenza wa Raila Odinga, mjadala uliibuka mitandaoni huku baadhi ya waenya wakimpongeza Raila kwa kumchagua Karua.

Baadhi ya viongozi kutoka muungano wa Kenya Kwanza walimshambulia Karua.

Mgombea mwenza wake Ruto Rigathi Gachagua alikuwa miongoni mwa viongozi ambao walishambulia Karua  kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wake Raila.

Gachagua  akipigia debe naibu rais katika kaunti ya Nyeri alidai kwamba rais Kenyatta alishindwa kuwapeleka upande wa wapinzani wao, hivyo basi Martha Karua hataweza.

"Sasa huyu mama ametumwa na yeye akija hapa mtamwambia mlijipanga kitambo? Gachagua aliuliza wakazi wa Nyeri," 

"Akija mtamwambia kama rais wetu ambaye yuko kwa kiti alishindwa kutupeleka kwa kitendawili, huyu ataweza kweli mnaweza kubali?."

Huku gavana  wa Kitui Charity Ngilu akijibu video yake Gachagua alisema kwamba hastahili kura ya wanawake iwapo aheshimu wanwake.

“HUYO MAMA…” Sikiliza kwa makini wanawake wa taifa hili kubwa, kama hawezi kukuheshimu HASTAHILI KURA YAKO. Hebu fikiria jinsi angewatendea wanawake ikiwa, Mungu apishe mbali, angekuwa Naibu Rais. Wanawake, tusikasirike, TUMPIGIE KURA! @MarthaKarua anatuwakilisha sisi sote.

Ngilu alizidi kumpa kongole Karua kwa kuwa Naibu rais, huku akisema kwamba amewakilisha wanawake wote wa nchi ya kenya.