'Hatukuwasilisha karatasi zetu,'Irungu Kang'ata azungumza baada ya kunyimwa kibali na IEBC

Muhtasari
  • Irungu Kang'ata azungumza baada ya kunyimwa kibali na IEBC
  • Anasema hawakuwasilisha karatasi zao kwa vile muungano wa wawaniaji wao ulifungua kesi ya kupinga uhakiki wao
Seneta Irungu Kang'ata

Mwaniaji ugavana wa Murang'a Irungu kang'ata amefafanua kuhusu suala la uthibitishaji analodaiwa kuwa nalo na IEBC.

Kupitia kwenye ukurasa wake daktari wa falsafa katika sheria anasema kwamba hakuwasilisha karatasi zake kama inavyodaiwa kuripotiwa.

Anasema hawakuwasilisha karatasi zao kwa vile muungano wa wawaniaji wao ulifungua kesi ya kupinga uhakiki wao na hivyo walikuwa wakitafuta muda ili wachunguze pingamizi hilo kwanza kabla ya kuwasilisha karatasi zao kwa wakati ufaao.

"IEBC HAIKUkataa karatasi zetu au kukataa kutuidhinisha. Hatukuwasilisha karatasi zetu. Tulitafuta muda wa kusoma barua ya pingamizi iliyowasilishwa na muungano wa wagombea kupitia mwanasheria.Hatufungui shauri lolote.Tukishaisoma barua hiyo, tutawasilisha karatasi zetu." Aliandika Kang'ata.

Kang'ata ambaye anawania kwa tikiti ya UDA anatazamiwa kumenyana na Jamleck Kamau wa Jubilee na chama cha Wakulima Irungu Nyakera.