UDA inajiandaa kukataa matokeo ya kura za Agosti-Kioni adai

Muhtasari
  • ''UDA inajiandaa kwa ajili ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa  Agosti kwa sababu wanajua wameshindwa
  • Kila mwanasiasa amekuwa akipigia debe kiongozi wa muungano wake
Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Jeremiah Kioni
Image: Jeremiah Kioni /TWITTER

Huku ikisalia tu siku 60,ili uchaguzi ufanyike vigogo na wanasiasa wanazidi kutabiri nani haswa atakaye mrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Kila mwanasiasa amekuwa akipigia debe kiongozi wa muungano wake,huku siku hiyo ikisubiriwa sana na wananchi pamoja na wanasiasa wa mirengo miwili kati ya Azimio na UDA.

Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Jeremiah Kioni sasa anasema kuwa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinapanga kukataa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti iwapo Azimio la Umoja anayepeperusha bendera Raila Odinga atashinda urais.

Kioni ambaye alikuwa akizungumza mjini Nyeri wakati wa mkutano na wagombeaji wa Jubilee mnamo Jumatano, alisema kuwa kambi inayoongozwa na Naibu Rais William Ruto tayari imeanza kuhisi kushindwa kutokana na ubashiri wa wachambuzi wa hivi majuzi.

''UDA inajiandaa kwa ajili ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa  Agosti kwa sababu wanajua wameshindwa.

Tunajitayarisha kama Jubilee Party kuhakikisha tunashinda kwa pengo kubwa ambalo kila mtu ataona anapoteza wakati wake,"Alisema.

Huku akionyesha imani kuwa chifu wa Azimio ndiye mshindi wa uhakika wa kinyang'anyiro cha urithi wa Rais Uhuru Kenyatta, Kioni, hata hivyo, alipuuzilia mbali mipango inayodhaniwa kuwa ya UDA, akisema kuwa kura za viongozi hao wawili zitakuwa tofauti kuwa wazi.

"Tofauti kati ya kura za Raila na Ruto itakuwa kubwa kiasi kwamba kila mtu ataweza kusema kwamba wanatupotezea wakati," alisema.