Ruto aeleza sababu ya kufika kwenye mkutano wa IEBC kuchelewa

Muhtasari
  • Ruto alisema Katibu Mkuu wake, Veronica Maina, alimweleza  kuwa kulikuwa na mabadiliko ya wakati wa mkutano huo
DP WILLIAM RUTO
Image: EZEKIEL AMING'A

Naibu Rais William Ruto alifika Jumatano akiwa amechelewa kwa mkutano wa Tume Huru ya Mipaka na wagombeaji urais.

Ruto alieleza kuwa haikuwa nia yake kuchelewa kufika, akisema mawasiliano ya awali yalionyesha mkutano huo ungeanza saa tano asubuhi.

Ruto alisema Katibu Mkuu wake, Veronica Maina, alimweleza  kuwa kulikuwa na mabadiliko ya wakati wa mkutano huo.

Alisema tayari alikuwa amepanga muda wa mikutano mingine saa za asubuhi hivyo basi kuchelewa kwake.

"Ningeomba labda katika siku zijazo, tupe notisi ya siku tatu hadi nne ili kutupa muda wa kutosha wa kujiandaa jinsi unavyoelewa Bw. mwenyekiti, kila dakika ni muhimu," Ruto alisema.

Awali Ruto alikuwa amepiga hema huko Tharaka Nithi ambapo alifanya mkutano wa jukwaa la uchumi wa kaunti.

Ruto aliandamana na Seneta wa Tharaka Nithi na ajenti mkuu wa United Democratic Alliance Kithure Kindiki.