Mtu asiyejulikana afyatua risasi kwa wanandoa wakigombana, aua mwanao na kumjeruhi mama

Wanandoa hao walikuwa wanagombana nje ya nyumba baada ya mama kukataa kuingia ndani ya nyumba.

Muhtasari

• Marehemu alitoka nje kumuangalia mama yao kabla ya mtu asiyejulikana kuwavizia na kufyatulia risasi kumuua papo hapo.

Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Image: YoutubeScreengrab

Polisi jijini Nairobi wameanzisha msako mkali dhidi ya jambazi mmoja anayeaminika kumiliki bunduki baada ya kufyatua risasi kwa wanandoa waliokuwa wakigombana usiku.

Katika tukio hilo lililotokea alfajiri ya Jumatano, gazeti la Nation linaripoti kuwa wanandoa hao walikuwa wanagombana nje ya nyumba baada ya mtu huyo asiyejulikana kuibuka na kuwafyatulia risasi, kupelekea kifo cha mwanao wanandoa hao.

Katika ripoti iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Kamukunji, wanandoa hao Cecilia Mugure, 42 na Njoroge Wahome, 47 walifika nyumbani kwao kutoka kula bata eneo la Bee Centre huko Umoja na kuanza kuzozana kwa sababu mwanamke huyo alikataa kumfuata mwanamume Kwenda ndani ya nyumba hiyo.

“Bi Mugure alijeruhiwa na mwana wa wanandoa hao, James Muriithi, 19, alikufa kwa majeraha ya risasi. Ndipo Bw Wahome aliponyoosha mkono simu yake na kumpigia binamu yake, Bw Karuri Karue, akimtaka akimbilie nyumbani kwake na kusaidia kuwakimbiza wawili hao hospitalini,” Nation waliripoti.

Ripoti ya polisi ilisema kwamba binti ya wanandoa hao ambaye ni dadake marehemu alieleza kuwa walisikia zogo kati ya baba na mama huyo iliyochukua zaidi ya saa mbili.

“Msichana aliwaambia polisi kwamba baba alipanda orofa wanaishi kwenye ghorofa ya pili na kumwacha mke nje. Alianza kunywa whisky na binti alipomuuliza baba alipo mama, hakujibu kamwe,” ripoti hiyo ilisema.

Hapo ndipo msichana huyo alimuamsha kakake mkubwa ili kuenda nje kumuangalia mama yao.

Wawili hao ndipo waliamua kumweleza dada yao mkubwa kilichokuwa kikiendelea. Kijana huyo alimwomba dada yake achukue simu yake kutoka nyumbani.

“Alikimbia hadi nyumbani na alipokuwa anarudi baada ya kuchukua simu, alisikia milio miwili ya risasi na akamuona wazi mtu akiwa ameshika bunduki. Hapo ndipo aliporudi haraka na kumjulisha baba yake kile alichokishuhudia,” ripoti hiyo ilisema kulingana na jarida la Nation.