Miguna Miguna atangaza kurejea Kenya Oktoba 20

Serikali ilipuuza agizo la mahakama kutomfurusha Miguna kutoka Kenya

Muhtasari

• "Ratiba ya kurudi nyumbani. Baada ya takriban miaka 5 ya uhamisho wa kulazimishwa, ninarudi nyumbani. Kuondoka Toronto: Oktoba 24, 2022. Nitawasili JKIA, Nairobi: Oktoba 25, 2022, saa mbili na dakika 20 usiku. Tutaonana, na kila mtu, " Miguna aliandika kwenye Twitter.

Miguna Miguna afurushwa kutoka Kenya mnamo Machi 2018
Miguna Miguna afurushwa kutoka Kenya mnamo Machi 2018
Image: MAKTABA

Miguna Miguna ametangaza rasmi kuwa atarejea Kenya mwezi ujao baada ya takriban miaka mitano akiwa uhamishoni.

Wakili huyo ambaye anaishi mjini Toronto Canada alisema atatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) asubuhi, Oktoba 20, 2022.

Awali kupitia ukurasa wake wa Twitter Miguna alikuwa amesema kwamba atarejea nchini tarehe 25 Oktoba kabla ya kubadilisha tena tarehe ya kurejea Kenya. 

"Ratiba ya kurudi nyumbani. Baada ya takriban miaka 5 ya uhamisho wa kulazimishwa, ninarudi nyumbani. Kuondoka Toronto: Oktoba 24, 2022. Nitawasili JKIA, Nairobi: Oktoba 25, 2022, saa mbili na dakika 20 usiku. Tutaonana, na kila mtu, " Miguna aliandika kwenye Twitter.

Tangazo hilo linajiri siku mbili baada ya Miguna kudai kupokea pasipoti mpya, akimpongeza Rais William Ruto kwa kufanikisha upatikanaji wa pasipoti yake.

Miguna alifurushwa kutoka Kenya mwaka 2018 baada ya kushiriki katika hafla ya kuapishwa kwa kinara wa upinzani Raila Odinga kama ‘Rais wa Wananchi’ katika bustani ya Uhuru Park.

Wakili huyo amejaribu mara kadhaa kurejea Kenya lakini juhudi zake zilitibuliwa na serikali ya rais Uhuru Kenyatta licha ya kuagizwa na mahakama kumhuruhu arejee Kenya.