Uganda yathibitisha visa vingine sita vya Ebola

Mtu mmoja amethibitiwa kufa kutokana na virusi hivyo.

Muhtasari

• "Hadi sasa, visa saba, na kifo kimoja, vimethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola aina ya Sudan," WHO ilisema katika taarifa yake.

Image: BBC

Visa sita vipya vya ugonjwa wa Ebola zimeripotiwa nchini Uganda kufikia sasa.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema Alhamisi, baada ya nchi hiyo kuripoti kifo chake cha kwanza kutokana na virusi vinavyoambukiza sana tangu 2019.

Wizara ya afya ya Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola katika wilaya ya kati ya Mubende siku ya Jumanne, na kutangaza kifo cha kijana wa miaka 24.

"Hadi sasa, visa saba, na kifo kimoja, vimethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola aina ya Sudan," WHO ilisema katika taarifa yake.

" Visa 43 vya mgusano vimetambuliwa  na watu 10 wanaoshukiwa kuambukizwa virusi hivyo wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mubende," WHO ilisema.

Hii sio mara ya kwanza kwa Uganda kuripoti visa vya Ebola ,kwani mwaka wa 2019 ugonjwa huo uliripotiwa na watu watano kufariki.

Watu walioambukizwa huwa hawaambukizi hadi dalili zionekane,baada ya  siku 21.

Kwa sasa hakuna dawa iliyoidhinishwa ya kuzuia au kutibu Ebola, ingawa aina mbalimbali za dawa za majaribio zinaendelea kutengenezwa na maelfu wamechanjwa nchini Uganda,Congo na baadhi ya nchi jirani.

Kulingana na wizara ya afya nchini humo ugonjwa huu unasambazwa kupitia maji ya mwili na kuenea kwa idadi kwa kasi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Wizara hiyo pia iliwarai wananchi kuwa watulivu na wawe macho wanapotangamana na wenzao na kuripoti haraka iwezekanavyo iwapo mmoja wao ataonyesha dalili kama vile homa, kutapika, kutokwa na damu, kuendesha,macho mekundu na maumivu ya koo.