Vikomo vinastahili kuvunjwa, Kipchoge asema baada ya kuvunja rekodi

Kipchoge sasa ameshinda marathoni 15 kati ya 17 za maisha yake.

Muhtasari
  • Muda ulikuwa kasi wa sekunde 30 kuliko ule alioweka mnamo Septemba 17, 2018 katika kozi hiyo hiyo huko Berlin
MWANARIADHA ELIUD KIPCHOGE
Image: ELIUD KIPCHOGE/TWITTER

Mwanariadha bora zaidi wa mbio za marathon duniani Eliud Kipchoge ametaja mafanikio yake mapya ya kikazi ya kuweka rekodi mpya ya dunia kama kikomo ambacho kilipaswa kuvunjwa.

Akitumia akaunti yake ya Twitter saa chache baada ya kufunga rekodi yake ya miaka minne kwa nusu dakika, Kipchoge alisema kuna mipaka ya kuvunjwa.

"Mipaka ipo ili kuvunjwa. Mimi na wewe pamoja," Kipchoge alisema.

Bingwa wa Olimpiki mara mbili alivunja rekodi yake ya dunia katika mbio za marathon za wanaume Jumapili mjini Berlin kwa kutumia 2:01:09 katika mwendo wa maili 26.2.

Muda ulikuwa kasi wa sekunde 30 kuliko ule alioweka mnamo Septemba 17, 2018 katika kozi hiyo hiyo huko Berlin.

"Ninaweza kusema kwamba nina furaha sana leo kwamba rekodi rasmi ya dunia iko kwa kasi tena. Asante kwa wakimbiaji wote ulimwenguni wanaonitia moyo kila siku kujitutumua," Kipchoge alisema.

Kipchoge sasa ameshinda marathoni 15 kati ya 17 za maisha yake.

Mnamo Oktoba 2017 baada ya kushindwa katika azma yake ya kutwaa rekodi mpya, bingwa huyo wa Olimpiki alisema angepanga kujaribu tena mwaka wa 2018.