Ababu Namwamba avunja kimya baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa michezo

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, mbunge huyo wa zamani wa eneo bunge la Budalangi alijawa na shukrani nyingi

Muhtasari
  • mbunge huyo wa zamani wa eneo bunge la Budalangi alijawa na shukrani nyingi kwa mkuu wa nchi kwa kumteua katika baraza lake la mawaziri

Aliyekuwa katibu mkuu wa utawala (CAS) katika utawala wa rais wa zamani Uhuru Kenyatta Bw Ababu Namwamba amejitokeza kutoa taarifa yake ya kibinafsi kufuatia hatua ya rais William Ruto kumteua nafasi ya juu serikalini.

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, mbunge huyo wa zamani wa eneo bunge la Budalangi alijawa na shukrani nyingi kwa mkuu wa nchi kwa kumteua katika baraza lake la mawaziri.

Namwamba aliteuliwa kuwa waziri katibu ajaye wa masuala ya vijana, michezo na sanaa katika kile kitakachomfanya achukue wadhifa huo kutoka kwa balozi Amina Mohamed ambaye amekuwa akihudumu katika wadhifa sawia katika awamu ya mwisho ya utawala wa Uhuru Kenyatta.

"Shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais William Ruto kwa imani na imani ya kuniteua kuwa Waziri wa Masuala ya Vijana, Michezo na Sanaa," aliandika.