Moses Kuria ateuliwa waziri wa Viwanda na Biashara

Kuria anachukua hatamu hizo kutoka kwa waziri Betty Maina

Muhtasari

• Itakumbukwa kuwa Kuria ndiye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kabisa kuwahi kutangaza kukubali matokeo ya ugavana Kiambu.

Moses Kuria atangaza kufunga akaunti yake ya Facebook
Moses Kuria atangaza kufunga akaunti yake ya Facebook
Image: Facebook

Aliyekuwa mbunge wa Gatunde Kusini Moses Kuria ambaye ni kiongozi wa chama cha kazi ameteuliwa kuwa waziri wa biashara na viwanda.

Katika tangazo hilo ambalo rais Ruto aliweka wazi alasiri ya Jumanne katika ikulu ya Nairobi, Kuria alitangazwa kuwa waziri wa wizara hiyo ambayo likuwa imeshikiliwa na Betty Maina.

Kuria alikuwa mtetezi mkuu wa sera za rais Ruto kipindi akiwa naibu rais na mgombea wa urais na uteuzi wake kama waziri wa Maendeleo ya Viwanda na Biashara ni jambo geni kwa wengi kwani hakuwa anategemewa kabisa.

Itakumbukwa kuwa Kuria ndiye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kabisa kuwahi kutangaza kukubali matokeo baada ya kugundua kwamba hakuwa na nafasi ya kushinda ugavana Kiambu.

 

Alikuwa anawania ugavana kupitia chama chake cha kazi dhidi ya aliyekuwa seneta, Kimani Wamatangi ambaye alishinda kwa tikiti ya chama cha UDA.