Ledama:Azimio inafaa kumteua Kanini Kega kwa EALA

Alikuwa mbunge wa Kieni kwa mihula miwili, akiwa mbunge pekee aliyechaguliwa tena 2017 katika Kaunti ya Nyeri.

Muhtasari
  • Katika taarifa yake Alhamisi, Ledama alidokeza kuwa Kega aliunga mkono bila kuyumba muungano wa Azimio wa Raila Odinga

Seneta wa Kaunti ya Narok Ledama Ole Kina amesema aliyekuwa Mbunge wa Kieni Kanini Kega anastahili kuteuliwa katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Katika taarifa yake Alhamisi, Ledama alidokeza kuwa Kega aliunga mkono bila kuyumba muungano wa Azimio wa Raila Odinga.

"Tunahitaji kumtunza @kaninikega1 alisimama kidete na Azimio na sasa analipia. EALA inaweza kuwa kutua laini kwa kaka yangu kutoka Mt Kenya," aliandika.

Kega alikuwa miongoni mwa viongozi waliomuunga mkono Raila hadharani na kwa shauku kuwania urais katika uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo, alipoteza kiti cha ubunge alichokuwa akiteteaht kwa Njoroge Wainaina wa chama tawala cha UDA.

Alikuwa mbunge wa Kieni kwa mihula miwili, akiwa mbunge pekee aliyechaguliwa tena 2017 katika Kaunti ya Nyeri.

Kega alikubali kushindwa kabla ya matokeo kutangazwa na akasema anaendelea kujaribu mambo mapya maishani.