Mamia ya viti tupu Uhuru Gardens yazua gumzo mitandaoni, huku taifa likisherehekea mashujaa

Tofauti na siku za nyuma, siku hii ingeshuhudia Wakenya wengi wakikusanyika kumsikiliza rais.

Muhtasari

• Alipungia mkono umati wa watu waliokuwa na furaha wakiimba jumbe za kumkaribisha alipokuwa akizungushwa uwanjani huku akisindikizwa na msafara wa rais.

Siku ya mashujaa ilikuwa iliandaliwa huku ukumbi ukiwa ukitarajiwa kuhudhuriwa na halaiki ya watu, ila kukawa sivyo.

Ukumbi huo kulionekana viti tupu hata baada ya kuwasili kwa Rais William Ruto, ambaye aliongoza hafla hiyo.

Taswira iliyoko kwenye ukumbi huo ni mwonekano wa viti kwenye uwanja vikiwa tasa huku vingine vikionekana vimerundikwa pamoja, huku baadhi ya waliohudhuria wakijishughulisha kwa kukaa kwenye viti vilivyopangwa pamoja.

Tofauti na siku za nyuma, siku hii ingeshuhudia Wakenya wengi wakikusanyika kumsikiliza rais.

Hapo awali, Ruto na mke wa rais wa Kenya Rachel Ruto walifika kwa sherehe hizo.Akiwa amevalia suti nyeusi na tai nyekundu, Ruto aliingia kwenye sherehe hizo kwa gari lake la Land-Rover.

Alipungia mkono umati wa watu waliokuwa na furaha wakiimba jumbe za kumkaribisha alipokuwa akizungushwa uwanjani huku akisindikizwa na msafara wa rais.

Hii ni sikukuu ya kwanza ya kitaifa kwa Ruto kama mkuu wa nchi na Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya.