Maafisa 5 wa polisi wa SSU watazuiliwa hadi Jumatatu - Mahakama

Watano hao wamefikishwa mahakamani kuhusiana na kutoweka kwa raia wawili wa India na dereva wao.

Muhtasari
  • Hakimu mkuu wa mahakama ya Kahawa aliamuru kwamba ataamua Jumatatu ikiwa watano hao watazuiliwa kwa siku 30 zaidi zilizoombwa na serikali kuruhusu uchunguzi ufaanyike
Image: ANDREW KASUKU

Maafisa watano wa polisi kutoka kitengo cha SSU kiliyovunjiliwa mbali na Rais Ruto watazuiliwa katika kituo cha polisi cha Industrial area  hadi Jumatatu watakapofikishwa mahakamani tena.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Kahawa aliamuru kwamba ataamua Jumatatu ikiwa watano hao watazuiliwa kwa siku 30 zaidi zilizoombwa na serikali kuruhusu uchunguzi ufaanyike.

Watano hao wamefikishwa mahakamani kuhusiana na kutoweka kwa raia wawili wa India na dereva wao.

Mahakama itaunganisha kesi na ya maafisa wengine 4 waliofikishwa mahakamani awali kuhusiana na suala sawa.

Wakili wao Danstan Omari alidai kwamba wateja wake waliteswa walipokuwa kizuizini katika kituo cha polisi cha Industrial area.