Kama rais anafanya kazi nzuri, aendelee hatuwezi kumtoa baada ta awamu 2 - MP Yakub

Hatutaki tufanye makosa ambayo tulifanya wakati wa Mwai Kibaki, tunamtoa kama hajamaliza kazi - Yakub.

Muhtasari

• Mtu akifikisha miaka 75 ndio hawezi ruhusiwa kuwania tena - Mbunge Salah Yakub.

Mbunge wa Fafi, Salah Yakub amejipata kaika jungu la mjadala baada ya kusema kuwa yeye na wabunge wenzake wanaazimia kupeleka mswada bungeni ili kujadili kuondolewa kwa kipenge cha katiba kinachomruhusu rais kuongoza kwa awamu mbili pekee.

Mbunge huyo alisema kuwa atawasilisha mswada bungeni ili kuona kwamba kipengele hicho kinafutiliwa mbali na badala yake kubadilishwa na kipengele cha umri wa rais atakayekuwa akihudumu madarakani.

Yakub alitolea mfano kwa kuseam kuwa yeye na watu wake wa Fafi wamefurahia uongozi wa rais Ruto ambao amewateua watu kazi mbali mbali pasi na kuangalia maeneo.

Alisema kuwa azma yake ya kuwasilisha mjadala huo kwenye bunge kulikwepesha taifa hali kama ile ya rais hayati Mwai Kibaki aliyelazimika kuondoka madarakani kutokana na awamu zake mbili kukamilika kisheria huku akiachia njiani baadhi ya miradi yake aliyokuwa ameianzisha.

“Hatutaki tufanye makosa ambayo tulifanya wakati wa Mwai Kibaki, tunamtoa yeye kazi kabla hajamaliza programu zake. Aliacha kiti kwa ajili ya katiba ya awamu mbili. Mimi na wabunge wenzangu tuko na mjadala unaoendelea sasa hivi, na mjadala wenyewe tunataka kuwaambia Wakenya ya kwamba mambo ya awamu mbili haiwezi kuwa sahihi, tunataka mjadala wenyewe ukuwe wa umri. Mtu akifikisha miaka 75 ndio hawezi ruhusiwa kuwania tena. Kwa hiyo tunawaambia matakwa makubwa ya mtu kuwania urais isiwe ni kufungiwa nje kwa awamu mbili bali umri,” mbunge Yakub alisema.

“Isiwe awamu mbili tatu au nne, kwa vile nchi ambazo zinaendelea kama German Merkel alikaa pale miaka karibu 20. Kwa hiyo sisi kuna mswada ambao tunaleta kwenye bunge tunasema hiyo mambo ya awamu mbili haitufai, kama rais anafanya kazi nzuri aendelee, hatuwezi kumtoa kabisa,” aliongeza.